GWIJI WA FILAMU SANJAY DUTT AAHIDI KUIPAISHA SEKTA YA FILAMU TANZANIA


UJIO wa Msanii nguli wa Filamu kutoka nchini India Sanjay Dutt unatarajiwa kuinufaisha sekta hiyo nchini baada ya kuahidi kushirikiana na Serikali katika kuboresha maeneo mbambali ndani ya sekta hiyo.

Msanii huyo aliyewasili nchini wiki iliyopita kwa ushirikiano baina ya Serikali na Kampuni ya vifaa vya umeme ya Kilimanjaro Cables (AFRICAB) na kupata fursa ya kukutana na viongozi mbalimbali wa kitaifa amesema atatumia nafasi yake kuhakikisha sekta ya filamu hapa nchini inapiga hatua ya juu zaidi.

Akizungumza na wasanii mbalimbali wa filamu katika semina maalumu yenye lengo la kubadilishana uwezo, nguli huyo alisema  mipango yake ni kushirikiana na wasanii wa hapa nchini kuandaa filamu mbalimbali jambo litaloweza kuwafanya kupiga hatua kimataifa.

Alisema pamoja na hilo kupitia ziara hiyo amesema atashirikiana na waandaaji na watengenezaji wa filamu nchini kwa ajili ya kuhakikisha filamu wanazoziandaa zinakuwa zenye ubora jambo litalosaidia sekta hiyo kukua.

Awali kabla ya kuzungumza na wasanii hao, Sanjay Dutt alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye aliupongeza ujio wake na nia yake ya kutaka kushirikiana na wasanii wa hapa nchini ili kuikuza sekta ya filamu.

Waziri Mkuu alisema kitendo cha msanii huyo kuonyesha dhamira yake ya kutaka kuwapa mbinu waaandiaji wa filamu kwa kuwaunganisha na waandaaji wa filamu wa nchini India, kitaongeza tija katika sekta hiyo nchini sanjari na wasanii kwa ujumla.

"Kupitia ujio wa msaani huyu inapaswa kuwa fursa kwa wasanii wetu kuona ni namna gani watatumia fursa hiyo kupata ujuzi wake na kuutumia kukuza vipaji vyao hivyo kulitangaza soko la filamu nchini" alisema Waziri Mkuu Majaliwa

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa alisema kwa kushirikiana na msanii huyo wataangalia maeneo ya kimkakati kwa kubadirishana uwezo na hivyo kupanua wigo wa masoko kwa filamu za Tanzania

Aidha alisema wamekubaliana na msanii huyo kuhakikisha wanakitumia chuo cha Sanaa Cha Bagamoyo (Tasuba) kukuza Sanaa hiyo ya filamu kupitia wataalam wabobezi kutoka nchini humo ambao watakuja kutoa mefunzo ya uandaaji wa filamu hizo. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kambuni ya AFRICAB ambao ndiyo wawezeshaji wa ujio wa msanii huyo, Yusuf Ezzi alisema lengo la kumleta msanii huyo nchini ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kuitangaza tanzania kupitia utalii.

Alisema kupitia ziara na filamu yake ya Rais ya Royal Your, kutaisaidia Tanzania kutangaza vivutio vyake huku ujio wa msanii Sanjay Dutt ukiunga mkono hatua hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments