SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MASOMO YA ZIADA KWA WANAFUNZI KIPINDI CHA LIKIZO 'WAPUMZIKE, TUNAWAHARIBU KUSOMA MUDA WOTE'

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Ummy Mwalimu amewaagiza wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wote nchini kuhakikisha wanasimamia suala la wanafunzi kupumzika wakati wa likizo ili kuwapatia watoto muda wa kujifunza masuala mengine ya kijamii.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo baada ya kupata maelekezo ya kisera kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknojia, Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako ambaye amemtaka kulisisitiza suala hilo ili wanafunzi hao waweze kupata muda wa kupumzika kipindi cha likizo.


Akihutubia kwenye Mahafali ya 29 ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo,Waziri Ummy amesema watoto wanatakiwa kupumzika majumbani kipindi cha likizo ili waweze kusaidia kufanya kazi ndogondogo nyumbani, kusoma dini na kusaidia kufanya biashara ndogo za kuwasaidia wazazi pale wanapokuwa likizo.


“Sasa hivi elimu imegeuzwa kama biashara, watoto wamekuwa wakisoma masomo ya ziada mpaka kipindi cha likizo, hawapumziki, pia wazazi huchangia fedha kwa ajili ya masomo hayo ya ziada, watoto hawafaulu kwa kusoma muda mrefu, hivyo nawaagiza wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanalisimamia hili,” amesisitiza Waziri Ummy.

Amesema, Serikali imepanga muda wa vipindi wa saa nane, ikiamini muda huo wanafunzi wataweza kujifunza kwa kina masomo yote yaliyopangwa kwa siku, hivyo amewataka Wakurugenzi kuwaelekeza wakuu wa shule kusitisha masomo ya ziada mpaka saa mbili usiku Jumatatu hadi Jumapili.

"Ninaagiza kusitishwa mara moja kwa kuwa hatuwajengi watoto,tunawaharibu kwa kuwachosha kusoma muda wote bila kupata muda wa kupumzika,"amesema Waziri.

Chanzo - Dira Makini Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

2/Post a Comment/Comments

  1. Tunaoongeza uamuzi wa kupiga marufuku masomo ya ziada kwa wanafunzi maana ilijenga matabaka na ukatili mkubwa kwa walioshindwa kumudu gharama za malipo. EDF tulipambana na hali hii bila mafanikio. Mungu amesikia.

    ReplyDelete

Post a Comment