Breaking

Post Top Ad

Tuesday, November 16, 2021

NGURUWE ABAKWA AKIWA AMEFUNGWA KAMBA AKISUBIRI KUCHINJWA


Mkazi wa kijiji cha Mavanga kilichopo katika kata ya Mavanga wilayani Ludewa mkoani Njombe anayefahamika kwa jina la Afro Nyigu (31) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumbaka mnyama aina ya Nguruwe.

Afisa mtendaji wa kijiji hicho Ramadhani Kihanga amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 14 2021 ambapo mtuhumiwa huyo alifika katika machinjio ya wanyama hao huku akiwa amelewa na kukuta nguruwe akiwa amefungwa kamba kwa maandalizi ya kuchinjwa ndipo kijana huyo alimvamia na kufanya nae mapenzi.

Amesema wakati akiendelea na tendo hilo mlinzi wa machinjio hiyo alikuwa ametoka kidogo na aliporejea alimkuta kijana huyo akiendelea kufanya kitendo hicho ambapo alimkamata na kumpigia simu balozi na mtendaji wa kijiji ambao walifika katika eneo hilo la tukio.

Amesema kuwa walipomuhoji kijana huyo sababu za kufanya kitendo hicho alidai ni maamuzi yake binafsi hivyo hapaswi kuulizwa ambapo viongozi hao wakamchukua na kumkabidhi mikononi mwa polisi.

“Kitendo alichokifanya huyu kijana mwenzetu ni cha kusikitisha sana! Tunaomba sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wengine maana kama ameweza kufanya hivi kwa mnyama anaweza kufanya uharibifu hata kwa binadamu”,amesema Kihanga.

Akizungumza kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Njombe Hamiss Issa na mtandao huu amesema ni kweli tukio hilo lipo na kwa sasa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa tukio hilo na mtuhumiwa amehifadhiwa katika kituo cha Polisi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages