CCM YAMTEUA SHANGAI KUGOMBEA UBUNGE NGORONGORO, GULAMHAFEEZ MUKADAM, MASUMBUKO KUGOMBEA UMEYA SHINYANGA


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa imekutana katika kikao maalum Jumapili 7 Novemba, 2021 Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Ndugu Emmanuel Lekishon Shangai kuwa mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Ngorongoro katika uchaguzi

mdogo utaofanyika tarehe 11 Disemba, 2021 kufuatia kifo cha Marehemu William Tate Ole Nasha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo.

Kamati Kuu imewateua Ndugu Gulamhafeez Abubakar Mukadam na Ella's Ramadhani Masumbuko kugombea kiti cha Umeya katika Manispaa ya Shinyanga.

Katika hatua nyingine kamati kuu imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ya ujenzi wa taifa Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.

Kamati Kuu imempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kutimiza mwaka mmoja tangu kuingia madarakani kuwa Rais wa nane wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kuendeleza mshikamano, kulinda tunu ya Umoja, Amani, utulivu sambamba na utekelezaji makini na imara wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020 - 2025.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments