BIASHARA UNITED, NYAMONGO SC WATOKA SARE BONANZA LA BARRICK NORTH MARA


Timu ya Biashara United imelazimika kutoka sare ya bila kufungana na Nyamongo SC, katika mchezo wao wa kirafiki uliochezwa kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Nyamongo wilayani Tarime katika Mkoa wa Mara, katika bonanza lililoandaliwa na mgodi wa Barrick wa North Mara.

Mechi hiyo ilihudhuriwa na wananchi wengi kutoka vijiji jirani na Nyamongo ambapo timu zote zilionesha mchezo mzuri huku Nyamongo FC ambayo ilijumuisha wachezaji kutoka Barrick ikicheza kwa kujihami kuhakikisha haipotezi mchezo huo dhidi ya timu hii kubwa nchini.

Baada ya jitihada za kila timu kuona lango la mwenzake kushindikana, iliamriwa ifuatiwe na hatua ya kupiga mashuti ya ‘penalty’ lakini ilishindika kufuatia mashabiki kuvamia uwanja huku wakazi wengi wa mji mdogo wa Nyamongo wakieleezea kufurahia matokeo hayo.

Akifungua mchezo huo wa kirafiki Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mnjentele, alisema michezo hujenga afya na kudumisha undugu, alielezea kufurahia kuona timu ya Biashara ambayo imefikia kushiriki ligi kuu nchini, ikicheza na timu ambazo zipo daraja la chini na aliipongeza Barrick mara kwa kuandaa bonanza hilo.

Lengo la bonaza hilo lilikuwa ni kudumisha shirikiano baina na jamii wafanyakazi wa mgodi na vijiji jirani ,kuunga mkono jitohada za Serkali kuhamasisha wananchi kuhusiana na maradhi kiwemo kupata chanjo ya UVIKO-19 na kupima virusi vya UKIMWI sambamba na kukuza vipaji vya vijana katika michezo.

Awali katika shughuli za utangulizi wa mechi hiyo, viongozi na wachezaji wa Timu ya Biashara United Mara walitoa semina elekezi kwa vitendo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mchezo huo kwa Nyamongo Football Academy inayoundwa na watoto wenye umri kati ya miaka 13 na 16.

Mgodi wa Barrick North Mara unapakana na vijiji 11 ambavyo vimekuwa vikinufaika kwa namna tofauti kutokana na kuwepo uwekezaji huo hususani katika miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu ya barabara, shule na vituo vya afya.

Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mnjentele akikagua timu
Mgeni rasmi (katikati) akiwa katika picha na wachezaji
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick wakingalia mechi hiyo
Wachezaji wakionyeshana ubabe wa kisoka katika mechi hiyo
Wachezaji wakionyeshana ubabe wa kisoka katika mechi hiyo
Wananchi wa eneo la Nyamongo wakifurahia mchezo huo
Wananchi wakijiandikisha kupima afya katika uwanja huo
Viongozi wa timu hizo wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza mechi
Wananchi wa eneo la Nyamongo wakifurahia mchezo huo
Wananchi wa eneo la Nyamongo wakifurahia mchezo huo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments