TIC NA ZIPA ZAHAMASISHA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI SEKTA YA UTALII

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na  Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) wanashiriki   maonesho ya Kwanza ya Utalii ya Kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  yanayoendelea jijini Arusha hadi tarehe 16 Oktoba, 2021  kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji na kueleza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania. 

Wananchi, wawekezaji na viongozi mbalimbali wametembelea katika banda la TIC na ZIPA na kupatiwa maelezo mbalimbali waliyohitaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Dkt. Maduhu I. Kazi  amefika katika banda la TIC na ZIPA na kuwahudumia wananchi mbalimbali waliofika katika banda hilo kwenye maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo  Oktoba 10,2021
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Dkt. Maduhu I. Kazi akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) katika banda la TIC na ZIPA  kwenye maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Arusha.
Waziri wa Wizara ya Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Musa ametembelea katika banda la TIC na ZIPA na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuitangaza Tanzania na Zanzibar kwa Wawekezaji katika maonesho ya kwanza ya Utalii ya Kikanda ya Jumuiya ya Africa mashariki yanayoendelea jijini Arusha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments