Breaking

Post Top Ad

Thursday, October 14, 2021

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Laongeza safari zake za ndani na nje ya nchi


Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeongeza safari zake za ndani na nje ya nchi, kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.
 
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa  ATCL  Josephat Kagirwa amesema  safari zilizoongezwa ni pamoja na za Dodoma- Mwanza, Dar es Salaam – Mtwara,  Dar es Salaam – Bujumbura,  Dar es Salaam – Lubumbashi pamoja na Dar es Salaam  – Nairobi.
 
Kagirwa amesema ongezeko la safari hizo ni linatokana na ujio wa ndege mbili hivi karibuni na ni  utekelezaji wa mpango mkakati wa shirika hilo,  ambapo lilijipanga  kupanua safari zake kwa kuongeza ndege.
 
Akizungumzia ujio wa ndege hizo  aina ya Airbus A220-300, Kagirwa  amesema zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 132, na kati ya hao 12 wa daraja la biashara na 120 daraja la uchumi.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages