SERIKALI YASHAURIWA KUHARAKISHA MCHAKATO WA UPATIKANAJI WA SHERIA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE


Na Dotto Kwilasa, Malunde 1 blog Dodoma.

SERIKALI imeshauriwa kuona haja ya kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa sheria ya bima ya afya kwa wote kwani itakuwa mwarobaini wa kusaidia wananchi kupata huduma za afya kwa uhakika na kuondosha ubabaishaji wa huduma hiyo kwa jamii.

Hayo yameelezwa  Jijini Dodoma na viongozi wa Kamati  ya dini mbalimbali pamoja na wadau wa afya    wakati wakichangia katika mkutano ulioandaliwa na Kamati hiyo  huku uliowakutanisha viongozi wa dini na wadau wa masuala ya afya.

Viongozi hao wa kamati ya dini mbalimbali wamesema kupitisha kwa sheria hiyo kutakuwa mkombozi kwa watanzania ambao wanakosa huduma za afya kutokana na kukosa fedha na wale wenye uchumi mdogo.

Akichangia katika mjadala huo, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Kanisa la Menonite, Nelson Kisare amesema Utafiti ulifanyika walipata  majibu na walitengeneza  kitabu na wnatumia  tafiti kushawishi serikali kuwa na sheria bora ambayo itakuwa inatoa haki kwa kila mwenye uhitaji

“Tumekuwa tukikutana mara kwa mara na kushauriana na leo tumekutana kuendeleza yale mazuri ni kitu gani kifanyike ili iwe ni kitu ambacho ni cha manufaa nipende kutoa shukrani kwa Serikali tumesikia katika hotuba za Rais akizungumzia Wizara ya fedha na Mipango  ilete fedha ili muswada huo uweze kupitishwa. Nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa juhudi hizi wanazofanya,”amesema.

Mwenyekiti huyo amesema lengo la mkutano ni nini kifanyike ili waweze kupata sheria ambayo itasaidia watu wenye kipato cha chini.

“Sasa tumekutana nini kifanyike ili tuwe na nia moja lengo moja tupime kwa pampja ili tupate sheria ambayo itatusaidia matumaini yetu ni kwamba tutajaliada kwa amani na upendo,”alisema.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata,Khamis Mataka amesema katika jamii kwa sasa hali ni mbaya hivyo inahitajika sheria ya bima kwa afya iweze kupita ili kuwakomboa watanzania wengi.

“Hali ya jamii ni mbaya tufanye mambo hii sheria iweze kupita ili ituletee nafuu watu wetu na sisi wenyewe,”alisema Mataka.

Kwa upande wake,Mratibu wa Kamati ya amani Taifa,Edmund Matotay alisema wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 vyama mbalimbali viliinadi sera ya bima ya afya kwa wote ambapo vilidai vikichukua Nchi bima ya afya kwa wote itaanza kutumika.

Alisema baada ya uchaguzi Rais( Hayati Dk.John Magufuli) alitamka Serikali ilete mchakato wa muswada wa bima ya afya kwa wote.

“Baadaye tulionana na Rais pale Ikulu akitamka Serikali ilete bima ya afya kwa wote sisi kama viongozi wa dini tulifurahi sana kwamba Rais ametamka jambo hilo,na katika hotuba Waziri wa Fedha na Mipango na wa Afya waliweka vifungu mbalimbali vya kulipia kaya maskini katika sheria ya bima ya afya kwa wote,”alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments