MENEJA ULINZI VODACOM APANDA KIZIMBANI KESI YA LENGAI OLE SABAYA


Meneja wa Ulinzi na Mshirika Katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama Vodacom PLC Makao Makuu, James Wawenje amepanda kizimbani leo Jumatano, Oktoba 20,2021 kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa mkuu wa Wilaya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake sita.

Shahidi huyo wa sita wa Jamuhuri akitoa ushahi wake mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama ya Arusha, Patricia Kisinda amesema idara yake ndiyo inahusika na mfumo wa kunakili kumbukumbu za kupiga na kupokea simu na kunakili ujumbe wa simu.

Akiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Ofmed Mtenga amesema idara yake pia ndiyo inahusika na kunakili kumbukumbu za kutuma na kupokea miamala.

Amesema amekuwa mwajiriwa wa Vodacom tangu Agosti 25, 2015 ma ana shahada uzamili masuala ya utawala katika ulinzi aliyoipata nchini Uingereza.

Amesema katika majukumu yake wateja wake wakubwa ni Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mahakama na taasisi zingine kama Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Mapato (TRA) na tume za ushindani.

Wawenje ameileza mahakama kuwa amekuwa akishirikiana kutoa taarifa za uchunguzi kwa mujibu wa sheria. Kusimamia ulinzi na mali za kampuni na kishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kutoa nyaraka zinapohitajika kwa mujibu wa sheria.

Katika shauri hilo la uhujumu uchumi namba 27, 2021 washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post