Breaking

Post Top Ad

Friday, October 29, 2021

MAYWEATHER AKATAA KUPIGA PICHA NA KIJANA ALIYEPAKA RANGI MAKUCHA


Mchezaji wa ngumi za kulipwa duniani Floyd Mayweather ameonekana akikataa kupiga picha (selfie) na kijana mmoja wa miaka 18 ambaye alikuwa amepaka rangi za kucha nchini Marekani.

Tukio lilitokea muda mchache baada ya kumalizika kwa mchezo wa kikapu kati ya Grizzlies dhidi ya Clippers uliofanyika katika uwanja wa Staples Center, ambapo kijana huyo alimfuata Myweather kwa ajili ya kupata picha ya pamoja lakini Floyd alipoona rangi katika kucha za kijana huyo alikataa kupiga naye picha.

Katika video inayosambaa mitandaoni ,Mayweather alisikika akisema ‘’ You got painted nails, I don’t take pictures with guys with painted nails (Umepaka kucha rangi, huwa sipigi picha na wanaume walipoka kucha zao rangi)”

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages