BARRICK YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA KUTOA MSAADA WA CHAKULA SHULENI, VITUO VYA WATOTO YATIMA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Sunday, October 17, 2021

BARRICK YAADHIMISHA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KWA KUTOA MSAADA WA CHAKULA SHULENI, VITUO VYA WATOTO YATIMA


Wanafunzi wakifurahia msaada wa chakula

**
Kampuni ya Barrick kupitia migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu iliyopo mkoani Shinyanga,imeadhimisha Siku ya Chakula kwa vitendo ambapo imetoa msaada wa chakula kwa shule zilizopo Nyang’wale, Kahama na Bugarama kwa ajili ya wanafunzi waliopo katika madarasa ya mitihani kupitia mpango wa kuongeza ufauluunaofadhiliwa na mgodi wa Bulyanhulu.

Pia kampuni ya Barrick imetoa msaada wa chakula kwenye vituo vya kulea watoto yatima vya Mvuma na Peace ambapo wafanyakazi wa kampuni walipata fursa ya kuwapata faraja watoto wanaolelewa katika vituo hivyo.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi msaada katika kijiji cha Bugarama na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale,Vitalis Ndunguru aliyepokea msaada kwa niaba ya shule za wilaya hiyo, kwa nyakati tofauti wameipongeza kampuni ya Barrick kwa uwezeshaji mbalimbali ambao Imekuwa ikifanya kwa jamii katika Maeneo yanayozunguka migodi yake na mkoa wa Shinyanga kwa ujumla.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akiongea wakati wa hafla ya kupokea chakula cha wanafunzi katika kijiji cha Bugarama.
Kaimu Meneja Mahusiano ya Jamii wa Bulyanhulu, Zuwena Senkondo akiongea katika hafla hiyo

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages