KUTANA NA JAMAA MWENYE WAKE 48 NA WATOTO ZAIDI YA 200...ANAJIITA MFALME WA SHETANI


Mganga wa miaka 81 kutoka Nigeria amewapa talaka wake zake 48 na kuapa kuwa hatooa tena maishani mwake.

Hata hivyo, Simon Odo Okoro almaarufu Onuwa na ambaye hujiita "mfalme wa shetani" amevunja kiapo hicho kwa kumwoa tena mmoja wa wake zake aliowapa talaka.

 Onuwa amemuoa tena mmoja wa wake zake aliowapa talaka, mwanamke wa miaka 18 kwa jina Chidinma.

Hata hivyo Onuwa amejitetea akisema kuwa msichana huyo ndiye aliyetaka kuolewa naye. 

Alisema: "Msichana huyo aliyenilazimisha nimuoe alikuwa amerejea kutoka Marekani. Alinisihi nimuoe ili anichunge nitakapozeeka.

 Yeye ni mwenyeji wa jimbo la Enugu.

 Kulingana na habari iliyochapishwa katika mtandao wa habari wa Vanguard, baadhi ya watoto wake walilala na baadhi wa wake zake. 

Aidha, baadhi ya watoto hao wanasemekana kula njama ya kumwua.

Onuwa ana wake 48 na watoto zaidi ya 200. Inaonekana Nigeria imejaliwa na wanaume wanaopenda kuoa wake wengi na kuzaa watoto wengi akiwemo Alhaji Masaba Belo aliye na wake 97 na zaidi ya watoto 200.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments