ACT WAZALENDO WAIBWAGA CCM JIMBO LA KONDE.... MOHAMED SAID ISSA ATANGAZWA MSHINDI

Mgombe Ubunge Mohamed Said Issa kupitia Chama cha ACT Wazalendo ametangazwa mshindi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo Konde kwa kupata kura 2391 huku mgombea wa CCM Mbarouk Amour Habib aliyepata kura 794 akifuatiwa na Salama Khamis Omar wa CUF aliyepata kura 98 na Hamad Khamis Mbarouk (AAFP) aliyepata kura 55 kati ya kura 3,338 zilizopigwa.

Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Konde Abdallah Said Ahmed amemtangaza Mohamed Said Issa leo Jumamosi Oktoba 9, 2021 katika kituo cha majumuisho cha Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments