Picha : MKUU MPYA WA MKOA WA SHINYANGA SOPHIA MJEMA AKABIDHIWA RASMI OFISI..ATAKA UWAJIBIKAJI

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akikabidhi nyaraka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Edward Mjema (kushoto) leo Jumanne Oktoba 12,2021 wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Edward Mjema amewataka viongozi wa serikali kuanzia ngazi za mitaa na vijiji kuwajibika kwa kusikiliza kero za wananchi ili kuleta maendeleo.

Mhe. Mjema ameyasema hayo leo Jumanne Oktoba 12,2021 wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina yake na aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo Dkt. Philemon Sengati.

"Ninataka Super Sonic Speed katika kuleta maendeleo kwenye mkoa wa Shinyanga. Ili kufikia maendeleo ni lazima kila mmoja awajibike. Nataka kuona vibe yaani nataka kuona mtetemeko wa Shinyanga", amesema RC Mjema.

"Viongozi kuanzia ngazi za mitaa tatueni matatizo ya wananchi, msikwepe majukumu yenu kwa kuogopa kuwa mtaonekana wabaya, msikae ofisini, lazima tukawatumikie wananchi..siku ya kupumzika ni siku ambayo utakuwa kwenye likizo yako, nenda kwa wananchi na tutapimana na kuulizana umefanya nini.... Lazima tuwe serious kuonesha kuwa Shinyanga inaendelea", amesema Mjema.

Amewataka viongozi kutokuwa sehemu ya migogoro katika jamii huku akiwataka viongozi kutatua matatizo ya wananchi badala ya kusubiri viongozi wa ngazi za juu waje.

Mjema amesisitiza kuwa atakuwa mkali kwa viongozi watakaotumia hovyo fedha za serikali na kwamba mtumishi wa serikali lazima awe mfano kwa wananchi kwa kuepuka mambo ya hovyo mtaani.

"Kiongozi wa serikali lazima uwe smart, uwe na nidhamu, kaa na nidhamu watu wakuone wewe ni kiongozi mwenye nidhamu. Tuwe na nidhamu, tuwajibike na tuwe mfano mzuri kwa wananchi..Ukiona pagumu nenda katafute pengine, Madam ushakuwa kiongozi wa serikali lazima uwe na nidhamu", amesema Mjema.

"Mhe. Rais Samia pia ametusisitiza kuachana na vitendo vya rushwa...Huku kwenye rushwa ndiko kwenye matatizo mengi, huku tutafanya kazi kubwa, kasafisheni nyumba zenu ili tuhakikishe kila tunapopita pako safi", ameongeza.

Mkuu huyo wa mkoa pia amesema hatapenda kuona mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga na kuwataka wananchi kuachana na imani za kishirikina huku akiwaomba viongozi wa dini na kimila kutoa elimu kwa wananchi kuachana na imani za kishirikina.

Soma pia : 

RC MJEMA : SHINYANGA TUNATAKA SUPER SONIC SPEED YA MAENDELEO..NATAKA VIBE!!

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akikabidhi nyaraka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Edward Mjema (kushoto) leo Jumanne Oktoba 12,2021 wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Edward Mjema wakisaini nyaraka za ofisi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Oktoba 12,2021 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Edward Mjema akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Oktoba 12,2021 

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Oktoba 12,2021 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Oktoba 12,2021
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Oktoba 12,2021
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Oktoba 12,2021
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Oktoba 12,2021
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Habib Makusanya akiomba dua wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Oktoba 12,2021
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Shinyanga Askofu Dkt. Emmanuel Makala akiomba wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo Jumanne Oktoba 12,2021

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Edward Mjema akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary (kushoto).

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments