Breaking

Post Top Ad

Monday, October 18, 2021

RADI YAUA NG'OMBE 15 TABORA
Ng'ombe waliokufa baada ya kupigwa na radi

Radi iliyoambatana na mvua imeuwa ng'ombe 15 usiku wa kuamkia leo Oktoba 18, 2021, katika Kijiji cha Zaire kilichopo Kata ya Ikomwa, Manispaa ya Tabora, ambapo ndani ya Zizi kulikuwa na ng'ombe zaidi ya 30.

Serikali ya wilaya ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda, imefika katika eneo la tukio kwa lengo la kuwapa pole wanafamilia.

Kufuatia hali hiyo serikali imeahidi kufanya tathmini kwa ajili ya kumshika mkono Homano Lugwesa, ambaye ni mmiliki wa ng'ombe hao.

Via EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages