WAZIRI MWAMBE AELEKEZA TIC KUJIKITA KUTOA ELIMU YA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe akisaini kitabu alipotembelea banda la TIC na ZIPA katika Maonesho ya Kwanza ya Utalii ya Kikanda ya Afrika Mashariki yaliyoanza leo tarehe 9 Oktoba, 2021 jijini Arusha.

****
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe ameshiriki ufunguzi wa Maonesho ya Kwanza ya Utalii ya Kikanda ya Afrika Mashariki yaliyohudhuriwa na nchi sita za Afrika Mashariki.

Katika ufunguzi huo uliofanyika leo tarehe 9 Oktoba, 2021 jijini Arusha, wafanyabiashara kutoka Misri wanaowakilisha Jumuiya ya Afrika-Asia (AFASU) nao wameshiriki na kutoa tuzo mbalimbali kwa ajili ya kuitambua Tanzania katika utalii kupitia Mlima Kilimanjaro.

Wafanyabiashara hao ni matokeo ya ziara iliyofanyika nchini Misri ambayo Mhe. Mwambe na Kituo cha Uwekezaji TIC waliifanya mwezi Juni, 2021 katika kuhamasisha uwekezaji kuja nchini.

Mhe. Mwambe ametembelea banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na kuelezwa mikakati iliyopo ya kuvutia na kurahisisha uwekezaji nchini.

Mwambe ameelekeza TIC kuhakikisha wawekezaji wanazijua fursa zilizopo na faida zake ili wafanye maamuzi yakinifu ya kuwekeza kwa faida ya nchi na yao.

Amesisitiza kuwa katika maonyesho haya ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Afrika Mashariki yanayoendelea kituo kihakikishe wawekezaji waliofika wanafahamishwa fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya utalii ili kuweza kuongeza uwekezaji katika sekta hiyo ambayo ni mojawapo ya sekta yenye mchango mkubwa katika pato la Taifa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Geoffrey Mwambe wanne kutoka (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji (ZIPA). Watatu kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji Uwekezaji – TIC, Bi. Anna Lyimo na wanne kutoka kushoto ni Bi. Farida N. Mohamed Meneja Uhamasishaji Uwekezaji – ZIPA katika maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Afrika Mashariki yaliyofunguliwa jijini Arusha leo 9 Oktoba, 2021
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji Uwekezaji Bi. Anna Lyimo (Kulia) akiwa na Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa TIC Bw. D. Liganda( Katikati) pamoja na Meneja wa Uhamasishaji Masoko ZIPA. Bi. Farida N. Mohamed wa kwanza (kushoto) kwenye ufunguzi wa maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika mkoani Arusha kuanzia leo tarehe 9 hadi 16 Oktoba, 2021.
Kaimu Meneja wa Idara ya Huduma kwa Wawekezaji Bw. George Mukono akitoa elimu kwa wateja waliofika kwenye banda kuhusu fursa za uwekezaji tulizonazo na namna ya kuwekeza nchini kwenye maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Jumuiya ya Africa mashariki yanayofanyika jijini Arusha kuanzia leo tarehe 9 hadi 16 Oktoba, 2021.
Kaimu Meneja wa Idara ya Huduma kwa Wawekezaji Bw. George Mukono wa tatu (Kushoto) akitoa elimu kwa wateja waliofika kwenye banda kuhusu fursa za uwekezaji tulizonazo na namna ya kuwekeza nchini kwenye maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Jumuiya ya Africa mashariki yanayofanyika jijini Arusha kuanzia leo tarehe 9 hadi 16 Octoba, 2021.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji Uwekezaji Bi. Anna Lyimo akitoa elimu kuhusina na majukumu ya TIC kwa watu waliofika kutembelea banda la TIC na ZIPA kwenye maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika mkoni Arusha kuanzia leo tarehe 9 hadi 16 Octoba, 2021.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments