Breaking

Post Top Ad

Monday, October 18, 2021

MTOTO WA DARASA LA TATU AOLEWA KWA MAHARI YA NGURUWE MMOJA


Mkazi wa Kitongoji cha Mabatini, wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Kennedy Fumpa (37), amekamatwa kwa tuhuma za kumuoa mwanafunzi wa darasa la tatu baada ya kulipa mahari ya Sh. 330,000 pamoja na nguruwe mmoja.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 11 (jina linahifadhiwa), alikuwa darasa la tatu na alilazimika kuacha shule baada ya bibi yake aliyekuwa akimlea kupokea mahari hiyo hivi karibuni na mjukuu wake kuhamia kwa mwanaume huyo ili wakaanze maisha ya ndoa ya mume na mke.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Godfrey Kalungwizi alisema serikali ya kijiji ilipata taarifa kutoka kwa uongozi wa shule kuwa mwanafunzi huyo amekuwa mtoro shuleni kwa muda mrefu ndipo jitihada za kumtafuta zikaanza.

Alisema baada ya jitihada za uongozi wa kijiji kumtafuta mwanafunzi huyo na kumbana bibi aliyekuwa anamlea, alieleza kuwa alikwisha pokea mahari na mjukuu wake huyo tayari amekwisha olewa.

CHANZO - NIPASHE

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages