Breaking

Post Top Ad

Monday, October 18, 2021

MWALIMU MKUU AMNG'OA JINO KWA KUMTWANGA NGUMI MWALIMU MWENZAKE MOROGORO


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkuyuni iliyopo katika Tarafa ya Mkuyuni Morogoro Vijijini anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumpiga hadi kumng'oa jino la juu mwalimu mwezake, Witnes Makoti huku chanzo kikiwa bado hakijulikani.

Mwalimu huyo aliyefahamika kwa jina la Mussa Hasira anadaiwa kutenda tukio hilo Oktoba 15,2021 baada ya kupishana kauli wakiwa shuleni hapo

Kamanda wa Polisi wa Polisi Morogoro, Fortunatus Musilimu amethibitisha kushikiliwa kwa mtuhumiwa.

Amesema kuwa, mtuhumiwa huyo alimshambulia kwa fimbo na ngumi mwalimu mwenzake huyo hadi kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages