JAMAA WA MIAKA 49 AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 6 - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Friday, October 1, 2021

JAMAA WA MIAKA 49 AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 6


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao
**
Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu, linamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 49, kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka sita kwa kile kilichoelezwa kuwa ni tamaa za kimapenzi.

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba Mosi, 2021, na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao, ambapo amesema tukio hilo limetokea Septemba 22, mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku Kitongoji cha Majengo, Kata ya Dutwa wilayani Bariadi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages