KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MISITU KUFANYIKA IRINGA NOVEMBA 10 -12, 2021



Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga akizungumza baada wa kuzindua maandalizi ya kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya misitu. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Saady Mtambule , Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Mohamed Moyo na kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Peres Magiri
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh Queen Sendiga akizungumza wakati wa uzinduzi wa maandalizi ya kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya misitu.

***

Mkoa wa Iringa ambao una miliki 40% ya misitu ya nchini Tanzania unatarajiwa kufanya Kongamano kubwa la wawekezaji na wadau wa sekta ya misitu tarehe 10 hadi 12 Novemba 2021. 

Akizindua maandalizi ya Kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga alisema " Mkoa wa Iringa ni kinara wa sekta ya misitu, na sasa Serikali ya Mkoa wa Iringa baada ya kuzindua mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa wa Iringa mwanzoni mwa mwaka 2021, sasa tunaleta kwenu kongamano hili la uwekezaji katika sekta ya misitu ambalo litaenda sambamba na maonesho ya sekta ya misitu na pia kongamano la wadau wa sekta hii’’.

"Pamoja na Mkoa wa Iringa kuwa kinara wa Sekta ya misitu lakini bado kuna fursa pana za uwekezaji na uanzishaji wa biasahra au huduma kwenye sekta ya misitu, Wilaya zote za Mkoa wa Iringa zimetenga aridhi kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya misitu hivyo Twenzetu Iringa, Misitu inalipa , Wekeza Sasa.’’,amesema.

Amesema wanatarajia Waziri Mkuu Mhe. MKassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano hilo la Uwekezaji katika sekta ya misitu. 

Kujisajili kwa ajili ya kongamano hili bonyeza link hii https://www.forestryinvestmentforum.co.tz.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments