Picha : HUHESO FOUNDATION, RUDI WAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UTOAJI RUFAA MATUKIO YA UKATILI WA KIJINSIA KWA KAMATI YA MTAKUWWA MWAKATA


Afisa Ustawi wa Jamii Kiongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala, Bw. Ignace Lufulila akizungumza kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Huheso Foundation kwa kushirikiana na RUDI Tanzania kwa ufadhili wa OXFAM Belgium wametoa mafunzo kuhusu Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya  Mpango Mkakati wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kata ya Mwakata halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo Alhamisi Oktoba 21,2021 katika ofisi ya Afisa Mtendaji wa kata ya Mwakata na kuhudhuriwa na Wajumbe wa MTAKUWWA kata ya Mwakata, maafisa wa Mashirika ya Huheso Foundation na RUDI Tanzania ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa Ustawi wa Jamii Kiongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala, Bw. Ignace Lufulila.

Awali akizungumza, Mratibu wa Mradi wa Kupunguza Athari za Maafa kutoka Shirika la Huheso Foundation ,Gerald Muheto amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo katika Halmashauri ya Msalala unaotelezwa na Shirika la Huheso Foundation kwa kushirikiana na RUDI Tanzania kwa ufadhili wa OXFAM Belgium.

“Leo tupo hapa kwa ajili ya Mafunzo kwa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata kuhusu Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa ajili ya kuchochea mapambano ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ndani ya jamii ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wetu wa Kupunguza Athari za Maafa (KAMA) katika kata za Shilela, Bugarama na Mwakata Halmashauri ya wilaya ya Msalala kwa ufadhili wa Shirika la OXFAM”,amesema Muheto.

“Tunatoa mafunzo haya baada ya kubaini kuwa matukio mengi ya Ukatili wa kijinsia yanayotokea Mwakata yanatokana na kwamba wajumbe wa kamati za MTAKUWWA hawana elimu kuhusu kukata rufaa ili kujua ngazi za kufuata katika kutatua kesi za matukio ya ukatili, mfano kesi za jinai hazipaswi kumalizwa kwa ngazi ya kijiji au kata bali zinatakiwa kupelekwa dawati la jinsia”,ameongeza Muheto.

Akizungumza katika kikao hicho Afisa Ustawi wa Jamii Kiongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala, Bw. Ignace Lufulila amesema matukio ya ukatili wa kijinsia yameendelea kuwepo kutokana na changamoto ya utoaji rufaa kuhusu matukio ya ukatili ambapo waathirika wamekuwa wakifanyiwa ukatili kutokana na kutojua wapi pa kupeleka kesi za matukio hayo.

“Tukio la ukatili linaweza kutokea lakini tusijue pa kulipeleka, sasa tunataka kujua wapi tupeleke kesi za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pindi yanapotokea. 

Miongoni mwa mambo ya kuzingatia unapotaka kutoa rufaa kwa mhanga wa matukio ya ukatili ni lazima kuzingatia mahitaji ya usalama, kisheria, kisaikolojia,kimwili,kitabibu na kiutamaduni. Wajumbe wa kamati za MTAKUWWA ni lazima wawe na mawasiliano na watu muhimu pindi tu yanapotokea ikizingatiwa kuwa matukio ya ukatili hayawezi kutatuliwa na mtu mmoja pekee”, amesema Lufulila.

Katika hatua nyingine Lufulila amewataka baadhi ya maafisa watendaji wa vijiji na kata na wajumbe wa MTAKUWWA kuwa waadilifu kwa kuepuka kugeuza kesi za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kuwa sehemu ya kitega uchumi kwa kuendekeza fedha na kuua kesi hizo.

“Wapo baadhi ya maafisa watendaji na wajumbe wa kamati za MTAKUWWA badala ya kukomesha matukio ya ukatili wao wakisikia kesi wanaanza kuongea na wahusika ili wamalize kesi, akipewa kitu kidogo kesi inaishia hapo.Kesi nyingi zinaishia kwa baadhi ya maafisa watendaji wa vijiji na kata, ukiona kapeleka kesi mbele ujue ameshindwa kuelewana na wahusika ili kumaliza kesi”,amesema

“Wana kamati za MTAKUWWA wanapaswa kuwa na fomu za rufaa hata hivyo niwakumbushe tu kuwa siyo kila kesi ni ya kupewa rufaa, zingine ni za kutoa ushauri inaishia hapo. Lakini matukio mengine ukiletewa tu hupaswi kuanza kuyasikiliza bali toa rufaa moja kwa moja mfano mtu kabakwa au kapigwa na kuumizwa.

Aidha amewataka wajumbe wa MTAKUWWA kufanya ufuatiliaji na kutoa rufaa kwa mtu akifanyiwa ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kuhamasisha jamii kutoa ushahidi kwa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto akisisitiza kuwa ili kutokomeza matukio ya ukatili wa jinsia ni lazima kuwepo ushirikiano kwa watu wote.

“Matukio ya ukatili ndugu zangu yanaumiza sana,madhara yake ni makubwa, unafurahi yakitokea kwa wengine lakini yakikufika wewe au ndugu yako ndiyo utaona namna gani yanaumiza sana. Msikae kimya mnapoona matukio,toeni taarifa, acheni tabia ya kwamba nikiripoti jirani ataninunia.Mme wangu akifungwa nani atatunza familia”,ameongeza.

Afisa Ufuatiliaji na Tathmini za Mradi wa KAMA unaotelezwa na Shirika la RUDI kwa usimamizi wa Shirika la OXFAM kwa ufadhili wa Serikali ya Ubelgiji, Leticia Shilinde amesema mradi huo unalenga kupunguza athari za Maafa katika jamii halmashauri ya Msalala akieleza kuwa Janga mojawapo ni ukatili wa kijinsia.

“Tunatekeleza mradi wa KAMA kwa kushirikiana na Huheso Foundation kwa kuzipatia elimu kamati za MTAKUWWA,kuangalia usalama wa watoto shuleni na kupiga vita mila na desturi na mila kandamizi zinazopelekea ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa za utotoni”,amesema.

Aidha amesema kamati za MTAKUWWA zinatakiwa kufanya kazi ya kutoa elimu kuhusu utoaji rufaa juu ya matukio ya ukatili wa kijinsia na kuiomba jamii kuacha kufika matukio ya ukatili

Mratibu wa Mradi wa Mwanamke Amka, unaotekelezwa na HUHESO kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society (FSC), Joyce Michael amewaomba wajumbe wa MTAKUWWA kujitoa kwa kutoa taarifa mapema na kufanya ufuatiliaji wa matukio ya ukatili wa kijinsia kwani wamepewa mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia

“Tuweni mabalozi wazuri, wajumbe wazuri, usikae kimya unaposhuhudia vitendo vya ukatili. Tusiwe na hofu ya kutoa taarifa kwani matendo ya ukatili wa kijinsia bado ni mengi sana katika jamii. Mabadiliko yanaanza na nyinyi mliopewa mafunzo, kukaa kimya ni dhambi”,amesema.

Naye Kaimu Mtendaji kata wa Mwakata William Emmanuel amewataka wajumbe wa kamati za MTAKUWWA kufuata taratibu na kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya ukatili huku akibainisha kuwa matukio ya ukatili yanaendelea kufanyika katika jamii kutokana na wanafamilia kumaliza kesi zao kienyeji.

Nao wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA akiwemo Salum Mohamed wamelishukuru Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania kwa kuwapatia mafunzo ya mfumo utoaji wa rufaa wa matukio ya ukatili wa kijinsia na kwamba yatapunguza madhara ya ukatili wa kijinsia na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Ustawi wa Jamii Kiongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala, Bw. Ignace Lufulila akizungumza kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania leo Alhamisi Oktoba 21,2021. Picha na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Afisa Ustawi wa Jamii Kiongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala, Bw. Ignace Lufulila akitoa mada kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.
Mratibu wa Mradi wa Kupunguza Athari za Maafa kutoka Shirika la Huheso Foundation ,Gerald Muheto akizungumza kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.
Mratibu wa Mradi wa Kupunguza Athari za Maafa kutoka Shirika la Huheso Foundation ,Gerald Muheto akizungumza kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.
Afisa Ufuatiliaji na Tathmini za Mradi wa KAMA unaotelezwa na Shirika la RUDI kwa usimamizi wa Shirika la OXFAM kwa ufadhili wa Serikali ya Ubelgiji, Leticia Shilinde akizungumza kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.
Afisa Ufuatiliaji na Tathmini za Mradi wa KAMA unaotelezwa na Shirika la RUDI kwa usimamizi wa Shirika la OXFAM kwa ufadhili wa Serikali ya Ubelgiji, Leticia Shilinde akizungumza kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.
Mratibu wa Mradi wa Mwanamke Amka, unaotekelezwa na HUHESO kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society (FSC), Joyce Michael akizungumza kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.
Mratibu wa Mradi wa Mwanamke Amka, unaotekelezwa na HUHESO kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society (FSC), Joyce Michael akizungumza kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.
Mjumbe wa kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata Salum Mohamed akilishukuru Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania kwa kuwapatia mafunzo ya mfumo utoaji wa rufaa wa matukio ya ukatili wa kijinsia
Kaimu Mtendaji kata wa Mwakata William Emmanuel akizungumza kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.
Katibu wa Baraza la Ardhi na Ndoa kata ya Mwakata, Amos Nengo Minze akichangia hoja kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.
Askari polisi kata Sajenti Wilson Batiani akichangia kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.
Mjumbe wa Kamati ya MTAKUWWA Kata ya Mwakata, Ashura Luhende Mayani akichangia kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.
Wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata wakiwa kwenye mafunzo ya Mfumo wa Rufaa kwa Waathirika wa Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kata ya Mwakata yaliyoandaliwa na Shirika la Huheso Foundation na RUDI Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments