BILIONEA JEFF BEZOS ATANGAZA MPANGO WA KUZINDUA KITUO CHA BIASHARA ANGANI


Picha ya Orbital Reef

Bilionea Jeff Bezos na mmiliki wa kampuni ya Blue Origin inayosimamia utalii wa angani ikishirikiana na kituo cha angani cha Sierra na Boeing imetangaza mpango wa kuzindua kituo cha biashara cha angani.

Kituo hicho 'Orbital Reef' kitakuwa na ukubwa wa futi 32,000 ambapo kitawawezesha wateja kuandaa filamu katika eneo hilo, kufanya utafiti na kutakuwa na hoteli ya angani.

Katika mkutano na wanahabari kuzindua mpango huo, maafisa wakuu wa Blue Originna kituo cha angani cha Sierra walikataa kutoa gharama ya ujenzi wa kituo hicho , ijapokuwa inadaiwa wanahakika kupata ufadhili wa kitita kikubwa kutoka kwa bwana Bezos, ambaye amejitolea kutumia $1bn (£726m) kwa mwaka katika kampuni ya Blue Origin.

Tangazo hilo linajiri huku Nasa ikitafuta mapendekezo ya kuunda kituo mbadala ili kuchukua mahala pake majengo ya kituo hicho yalio angani kwa miaka 20.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments