YANGA YANG'OLEWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, September 19, 2021

YANGA YANG'OLEWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  Malunde       Sunday, September 19, 2021

Vigogo,Yanga SC wamechapwa 1-0 na wenyeji Rivers United, katika mechi ya marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.

Yanga wanaaga mashindano hayo kwa kichapo cha jumla cha 2-0 kufuatia kuchapwa 1-0 Jumapili iliyopita katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Wawakilishi hao wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa, Yanga  jitihada zao za kupindua meza kimataifa zimekwama nchini Nigeria kwa kuwa wamefungwa tena.

Yanga ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi wa zaidi ya bao 1-0 kwa kuwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Leo pia ugenini nchini Nigeria Yanga imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 hivyo wametolewa kwa jumla ya mabao 2-0.

Safari yao na malengo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika imeyeyuka mazima hivyo wanarudi Dar es Salaam.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wamefanyiwa vitendo vya kihuni na wapinzani wao hasa kwenye suala la vipimo vya Corona.

"Tumefanyiwa mambo ya kihuni na tumepewa matokeo ya Corona dakika 45 kabla ya mchezo huu ni uhuni,".
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post