WANAOWAIBIA WAKULIMA WA ZAO LA DENGU KWA KUTUMIA VIPIMO FEKI KUONJA JOTO LA JIWE

Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Shinyanga Bw. Hilolimus Mahundi akionesha ndoo  zilizotanuliwa na moto zinazotumiwa na wafanyabiashara kuwaibia wakulima wa zao la dengu

*******
Katika kuhakikisha wakulima wazao la dengu katika halimashauri ya wilaya ya Shinyanga hawapunjwi na wafanyabiashara,  Wakala wa Vipimo mkoani Shinyanga (WMA), wameendelea kufanya ukaguzi wa mizani zinazotumika sehemu tofauti hasa kwa wanunuzi wa zao la dengu na kufanikiwa kukamata vipimo feki vinavyotumiwa na baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waadilifu kununua zao hilo. 

Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Shinyanga Bw. Hilolimus Mahundi amesema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kutaka kubaini mizani zisizo na viwango ambazo hazitoi kipimo kinachostahili.

Mahundi  amesema katika kuhakikisha wakulima wanauza mazao yao kwa kutumia mizani sahihi iliyohakikiwa na wakala hao wameweka utaratibu wakutoa elimu kwa wananchi pamoja na kufanya ukaguzi wakushtukiza ili kubaini wale wote wanao vunja sheria ili hatua kali ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

  “Nawapongeza wakulima wa zao la dengu katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga maana kwa sasa baada ya kupata elimu wamekuwa wakitoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa wafanyabishara wasiokuwa waadilifu wanaotumia ndoo zilizotanuliwa na moto kwa ajili ya kuwaibia wakulima,”amesema Mahundi.

Ameeleza kuwa, kwa Mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura 340, Wakala wa Vipimo ndiyo wenye jukumu la kusimamia usahihi wa vipimo vinavyotumika au vinavyotarajiwa kutumika kufanyia biashara kwa lengo la kumlinda muuzaji na mnunuzi.

Ameeleza kuwa kwa mtu yeyote atakayebainika akitumia vipimo visivyo sahihi kumuibia mkulima faini yake ni kuanzia shilingi laki 1 mpaka milioni 10.


Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Shinyanga Bw. Hilolimus Mahundi akionesha ndoo zilizotanuliwa na moto zinazotumiwa na wafanyabiashara kuwaibia wakulima wa zao la dengu
Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Shinyanga Bw. Hilolimus Mahundi akionesha ndoo zilizotanuliwa na moto zinazotumiwa na wafanyabiashara kuwaibia wakulima wa zao la dengu
Ndoo zilizotanuliwa na moto zinazotumiwa na wafanyabiashara kuwaibia wakulima wa zao la dengu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments