WAANDISHI WA HABARI WA GLOBAL TV , DAR MPYA WAPATA AJALI TABORA


Mwandishi wa habari wa Global TV, ambaye kituo chake cha kazi ni jijini Dodoma, Mohamed Zengwa (pichani chini) na wenzake wawili wamepata ajali mbaya ya gari leo Jumanne, Septemba 21, 2021 katika Kijiji cha Usimba, wilaya ya Uyui mkoani Tabora.

Zengwa na wenzake akiwemo dereva wa gari hilo na mwanahabari wa Dar Mpya, John Marwa, wamepata ajali hiyo baada ya gari aina ya Land Cruiser V8 lenye namba za usajili T 835 DRR walilokuwa wakilitumia kupasuka tairi ya nyuma na ya mbele ya upande wa kushoto na kusababisha gari hilo kupoteza uelekeo na kupinduka.

Watu wote watatu waliokuwa kwenye gari hiyo, hawajaumia sana zaidi ya kupata majeraha madogo madogo na hali zao zinaendelea vizuri ambapo wamekwenda hospitali kwa ajili ya vipimo matibabu zaidi.

Zengwa na wenzake hao, walikuwa wakisafiri kuelekea mkoani Kigoma kikazi.

Uongozi na wafanyakazi wote wa Global Publishers Ltd, tunawapa pole ndugu zetu hawa kwa ajali hiyo, pia tunamshukuru Mungu kwa kuwanusuru kutokana na ajali hiyo mbaya na tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awaponye majeraha waliyoyapata ili warejee kuungana na familia zao na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.

CHANZO - GP












Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments