RAIS SAMIA KUHUDHURIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Septemba 18, 2021 anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo tarehe 23 anatarajiwa kulihutubia baraza hilo.

Pamoja na Mkutano huo, Rais Samia pia atahudhuria  mikutano ya kilele ya kujadili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)

Aidha, anatarajiwa pia kukutana na wakuu wa nchi nyingine na viongozi wa mashirika ya kimataifa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi na taasisi zao.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments