RC MALIMA AITAKA TOC KUSHIRIKI MASHINDANO OLIMPIKI MWAKA 2024

 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akisistiza jambo wakati akifungua mafunzo ya walimu wa Mchezo wa Mpira wa Magongo yaliyoanza septemba 15 Jijini Tanga kwa kushirikisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani yakiratibiwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)na Chama cha Mpira wa Magongo Tanzania (THA) wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo
Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa Mchezo wa Mpira wa Magongo Tanzania Abdulrahman Syskes akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo 
Mkufunzi wa Kimataifa Maggid Muhamid Elati akieleza jambo
Mkufunzi wa Kimataifa Maggid Muhamid Elati akieleza jambo
Meza Kuu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mafunzo hayo
Picha ya Pamoja
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo

NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ameitaka Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kuhakikisha wanajiwekea malengo makubwa ya kuhakikisha timu ya Mpira wa Magongo inashiriki mashindano ya Olimpiki mwaka 2024 ili kutengeneza alama ya mchezo huo kama ilivyokuwa mengine.

Malima aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya walimuwa Mchezo wa Mpira wa Magongo  yaliyoanza septemba 15 Jijini Tanga kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Nyumbani kwa kushirikisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani yakiratibiwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)na Chama cha Mpira wa Magongo Tanzania (THA)

Alisema lazima watengeneze malengo ya lazima wajiwekee malengo makubwa yatakayokuwa na tija siku za usoni kwa kuhakikisha wanashiriki mashindano makubwa na wanafanya vizuri ili kuweza kuweka alama kubwa kupitia mchezo huo hapa nchini

“Ndugu zangu tuwe na malengo..Tujiwekee malengo makubwa ya kushiriki mashindano ya Olimpiki mwaka 2024 nafikria malengo ya muda mrefu na kati ni kushiriki huko na muda kufikiria ni sasa lazima mzingatie hilo na kuwa na maono ya mbali”Alisema

Alisema kwa sababu bila malengo itakuwa ni ndoto kuweza kufika huko hivyo ni lazima waweze kutengeneza alama kwenye mpira wa magogo kwani bila kufanya hivyo watakuwa wanapoteza muda lakini wakiutumia vizuri wanaweza kufika huko.

 “Lazima muanze kuota leo mpo Parisi bila malengo bila njozi tutapoteza muda mtafute kila mbinu ya kuwa walimu bora na hilo ndilo ambalo litatupa dira na mwanga mzuri wa kufikia kufikia malengo yetu ambao tunajiwekea ya kufika mbali”Alisema

Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo ambayo yatafanyika kwa siku 10 Jijini Tanga,Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Filbert Bayi alisema mafunzo hayo yalikuwa yafanyike mwaka jana lakini walilamika kuhairisha.

Alisema yalihairishwa kutokana na na taratibu za baadhi ya nchi waliona bado mapema kutoka nchi zao mfano Misri kumleta Mkufunzo wa Kimataifa Maggid Muhamid Elati kutokana na Covid 19 lakini walikubali baada ya chama kuwasailina nao nao wakakubali na mafunzo yaendelee.

Alisema mchezo wa Mpira wa Magongo ni mkongwe kwa sababu hakuna chama cha mchezo ambacho kimekwisha kushiriki mashindano olimpiki na timu pekee yenye wachezaji wengi kushiki olimipiki huku akieleza tokea mwaka 1980 mchezo huo umekuwa na mafanikio makubwa.

Katibu Mkuu huyo alisema kubwa ambalo hajalijua ni mashindano ya mikoa,vilabu ni muhimu sana lakini kwanini hakuna mashindano ya mkoa au vilabu kwa sababu zamani kulikuwa na vilabu vikubwa sana na nani atayayaleta mahindano ya Taifa na vilabu.

Alisema wameendesha kozi hiyo mwaka 2012 na  wameanza kufundisha kwenye uongozi wao tokea mwaka 2005 Zanzibar na 2021 wapo Jijini Tanga  ambayo ni mafunzo ya tatu hivyo kwa idadi kubwa ya walimu waliofundishwa TOC hivyo  wanategmea vyama husika Zanzibar na Bara vinawafuatilila na kuwatumia ipasavyo ili  kuinua kueneneza mchezo huo nchi nzima

“Badala ya mikoa michache tungependa mtakaporudi nyumbani vyama viendeleze na mkahakikisha mnashirikiana kwa lengo la kuhakikisha mchezo huo unaenea na kupendwa kutokana na ujuzi ambao mtakuwa mmeupata kwenye mafunzo hayo “Alisema Katibu huyo.

Aidha alisema idadi ya washiriki ni 30 walioiweka kutokana na gharama  na bajeti yao huku akieleza kwa muda mrefu TOC ,IOC imekuwa ikifadhili mafunzo ya michezo mbalimbali ya walimu wa vyama wanachama TOC ikwemo  Chama cha Mpira wa Magogo ambapo ni kati ya vyama vya michezo ambavyo vimefaidika na ufadhili huo .

Mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments