RUGEMALIRA AFUTIWA MASHTAKA...AACHIWA HURU


Mfanyabiashara James Rugemalira akiwa na familia yake nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Septemba 16,2021.
***
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) amefuta mashtaka yanayomkabili Mfanyabiashara James Rugemalira na mahakama kumwachia huru.

Juni 2017, Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nchini Tanzania TAKUKURU iliwafikisha Mahakamani Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth na Rugemalira kwa makosa sita ya uhujumu uchumi ikiwemo kosa la kuisababishia serikali hasara.

Aidha katika shtaka jingine, Washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Novemba 28/29, 2011 na Januari23,2014 makao makuu ya benki ya Stanbic Kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi St Joseph zote za Dar es salaam, kwa ulaghai, walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), USD 22,198,544.60 na shilingi 309, 461,300,158.27.

Iliendelea kudaiwa kuwa katika shtaka la kusababisha hasara, washtakiwa hao wanadaiwa kwamba mnamo Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la kati Kinondoni kwa vitendo vyao waliisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198, 544.60 na Tsh 309,461,300,158.27.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments