RAIS SAMIA AWAASA VIONGOZI ALAT KUTOA ELIMU YA UVIKO 19 | MALUNDE 1 BLOG

Monday, September 27, 2021

RAIS SAMIA AWAASA VIONGOZI ALAT KUTOA ELIMU YA UVIKO 19

  Malunde       Monday, September 27, 2021

 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa serikali za mitaa kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 kwa wananchi.

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi hao kutotumia mabavu katika utoaji wa chanjo bali kuwaelimisha wananchi wapate chanjo kwa hiari.

Rais ametoa kauli hiyo leo Septemba 27, 2021wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya serikali za mitaa- ALAT Taifa Mkoani Dodoma.

“Tulisema hili jambo ni la hiari, ukipita nyumba kwa nyumba anayetaka mchome asiyetaka usichome Lakini kubwa ninalotaka kusema mtu ana hiyari ya kukubali au kukataa na kama ana elimu ya kutosha ,hawezi kukataa”

Katika mkutano huo maalum Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi hao kushirikiana na kuondoa tofauti Zao ambazo nyingi hutokana na maslahi binafsi.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post