NHIF YAKUTANISHA WADAU KUFANYA TATHIMINI YA MIAKA 20



Mwenyekiti wa bodi wa NHIF Juma Muhimba akizungumza kuhusiana na na ushauri wa bodi unavyofanya kuweza kufanya vizuri katika utendaji ili kutoa huduma bora kwa wanachama, jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa umoja wa watoa huduma za afya Binafsi (AFTA) Dkt. Egina Makwabe akizungumza kuhusiana na mchango wao katika mfuko wa NHIF

Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es Salaam Hassan Rwaga akizungumza katika mkutano wa wadau wa watoa huduma za afya na NHIF kwa ajili ya kufanya tathimini ya miaka 20 uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bernad Konga akizungumza kuhusiana na mfuko huo tangu ulipoanzishwa na hatimaye kufika miaka 20 katika mkutano wa wadau wa Afya na NHIF uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Picha mbalimbali za washiriki wa mkutano kati NHIF na wadau wa watoa huduma za afya

*************************

*Katibu tawala Mkoa Dar es Salaam aipongeza NHIF kwa kuimarisha huduma



SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema kuwa itaendelea kutoa ushuirikiano kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika kuimarisha mfuko huo uendelee kufanya vizuri kwa kuongeza idadi wanachama la kufikia asilimia 50 ya dhamira Rais Samia Hassan Suluhu.

Hayo ameyasema Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Hassan Rwagwa wakati akifungua mkutano wa Watoa Huduma za afya na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutathimini mfuko huo kwa mafanikio miaka 20 tangu kuanzishwa kwa mfuko na kuangalia masuala mengine ya kufanya kufanya vizuri zaidi.

Rugwa amesema kuwa licha ya kufanya vizuri kwa mfuko watoa huduma wa afya wa serikali wanatakiwa kuwa tofauti katika utoaji wa huduma ili kufanya wananchi kuwa na imani na huduma za afya na kuachana mambo yasiyo mpendeza mteja.

''Miaka 20 ya NHIF kielelezo kuwa mmepita kwenye changamoto ambazo mliweza kuhmili na kusimamia mfuko katika kuweza kuwahudumia watanzania ambapo sasa bado mnaendelea katika maboresho mbalimbali ya kuujenga mfuko''amesema Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Sslaam Rugwa.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Bernad Konga amesema kuwa lengo la mkutanoni kuwashukuru Watoa Huduma za matibau kwa wanachama wa Mfuko huu kwa mchango mkubwa kwa taasisi hii kwa miaka hii 20 ya uhai wake.

''Hatuwezi kuhesabu mafanikio ya Mfuko huu bila kuhusisha kundi hili muhimu kwa Mfuko maana sisi ni kiungo tu kati ya Wanachama na Watoa huduma hawa na kuadhimisha miaka 20 ya NHIF kwa pamoja na Watoa Huduma za Afya kwa kuangalia kwa pamoja tulipotoka, tulipo na tunapoelekea huku tukiimarisha mahusiano baina yetu na kujenga dhana ya uwazi katika utendaji kazi wetu sisi kama Mfuko na Watoa Huduma'' amesema Konga.

Amesema mwendelezo wa kushirikisha kundi hili mara kwa mara umesaidia katika kuharakisha mafanikio ya kihuduma kwa wanachama na Mfuko umekuwa ukikitania na Watoa Huduma mara kwa mara kwa umoja wao, kupitia umoja wao na hata kimikoa kupitia ofisi zetu mikoani na kuendelea kupeana mrejesho ya yaliyofanyika katika kipindi chote hiki na kujadili kwa pamoja mambo mbalimbali yanayotuhusu katika kuhudumia wanachama wa Mfuko.

Amesema tumekuwa na mikutano ya mara kwa mara na hata mawasilsiano ya maandishi hasa panapotokea maboresho, changamoto na miongozo mbalimbali. Mathalani tunapofanya maboresho ya kitita cha mafao, huwa unawashirikisha Watoa huduma kama wadau muhimu katika hili.

Lengo kubwa la kuwashirikisha wadau wetu ni kuhakikisha wote kwa pamoja tunatembea tukizungumza lugha moja kwa nia ya kuwahudumia vizuri wanachama ambao wamechangia kabla ya kuugua.

Aidha amesema NHIF umewezesha vituo mbalimbali kuimarisha huduma za matibabu na miundombinu kupitia mikopo nafuu inayotulewa na NHIF. Vituo kama MNH, MOI, KCMS, BMH na vingine ni wanufaika.

Malipo kwa Watoa huduma kwa sasa yanalipwa ndani ya muda mfupi zaidi wa kati ya siku 30 hadi 45 ikilinganishwa na awali ambapo ilikuwa ni siku 60 na wakati mwingine kuzidi na kufikia 100. Aidha malipo hayo yamewezesha vituo kuwa na mapato ya uhakika ambayo yanawezesha vituo kuimarisha huduma.

Amesema NHIF imeboresha kitita cha mafao kwa wanachama wetu ambapo kwa sasa wanapata huduma nyingi zaidi zikiwemo za kitalaam na ambazo awali hazikupatikana hapa nchini ikiwemo huduma za figo.

Konga amesema wameimarisha utendaji kupitia TEHAMA, na kwa sasa ipo mifumo ya uchakataji na ulipaji madai, usajili wa wanachama, mifumo ya mawasiliano pamoja na kutanua uwigo wa upatikanaji wa huduma kwa wanachama kwa kusaijili zaidi ya vituo 8000 katika mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar na vituo hivi ni pamoja na vya serikali, binafsi, madhehebu ya dini na maduka ya dawa.

Hata hivyo amesema katika safari ya NHIF na Watoa huduma kwa miaka hii 20 zipo changamoto nzuri zinazoleta mafanikio ambapo kati ya hayo ni malalamiko ya watoa huduma kucheleweshewa malipo ya madai ao hali iliyofanya kuanzisha mfumo wa uwasilishaji, uchakataji na ulipaji wa madai kwa njia ya mtandao.

changamoto ya udanganyifu kwenye huduma na madai ya malipo kwa kuimarisha mifumo ya huduma kupitia TEHEMA mfano sasa hivi mwanachama anapata taarifa ya huduma alizopata kupitia simu zao mara baada ya huduma, pia tumeanzisha kitengo cha kushughulikia udanganyifu na tumeendelea kufanya support supervision.

Amesema Kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya wanachama kukosa huduma katika vituo ambazo zinalipiwa na Mfuko – Tumeendelea kutoa elimu kwa watoa huduma lakini pia kuchukua hatua kwa wanaofanya kinyume na makubaliano pia kuendelea kuimarisha mawasilisno na wanachama ili kupata taarifa kwa wakati.

Mfuko huo sasa umetimiza miaka 20 tarehe 1 Julai 2021. Tukiangalia tulipotoka ni mbali na tunayo mikakati ya tunapoelekea kama taasisi kwa kufikia wananchi wote na mpango wa bima ya afya (Bima ya Afya kwa Wote)kuendelea kuboresha huduma za matibabu kwakushirikiana na wadau ikiwemo Watoa huduma kuendelea kushiriki uimarishaji wa huduma za matibabu kwa kuwezesha vituo kupitia mikopo ya vifaa tiba na miundombinu.

kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Juma Muhimbi amesema kazi ya bodi ilitembelea na kuzungumza na watoa huduma wenu wa nchi nzima huku mkoa wa Dera es Salaam ukiwa na wa vituo vingi vya huduma kuliko mikoa yote, unawapa nafasi ya kufahamu na pia kuona hali halisi ya matibabu katika vituo vyetu vya kutolea huduma, hatua inayowapa mwanga zaidi katika utoaji wa maamuzi hususan mnapojadili namna ya uboreshaji wa huduma katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Muhimbi amesema uwepo wa vituo hivi ni ishara nzuri ya upatikanaji wa huduma kwa wanachama kiurahisi, lakini pamoja na uwepo wa vituo hivi bado naamini kuwa zipo changamoto za hapa na pale hivyo kupitia kikao hiki changamoto hizi zitajadiliwa na kufikia maamuzi ya pamoja ya namna ya kukabiliana nazo.

Amesema kwa upande wa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam tutaendelea kuwapa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha ndoto ya Serikali yetu ya upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wote inafikiwa. Tunaamini kwamba unapokuwa na wananchi wenye afya njema na uhakika wa matibabu unakuwa na uhakika wa kuzalisha zaidi na kufikia malengo ya Taifa huku azma ya serikali hii kufikia watanzania wote na huduma bora za matibabu kupitia bima ya afya kwa wote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments