WAFANYAKAZI 40 KIWANDA CHA NONDO MWANZA WANUSURUKA KIFO BAADA YA KINU CHA MOTO KULIPUKA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, September 25, 2021

WAFANYAKAZI 40 KIWANDA CHA NONDO MWANZA WANUSURUKA KIFO BAADA YA KINU CHA MOTO KULIPUKA

  Malunde       Saturday, September 25, 2021

Wafanyakazi wa kiwanda cha Nondo waliolipukiwa na uji wa moto

Wafanyakazi 40 wa kiwanda cha Nondo cha Nyakato jijini Mwanza, wamejeruhiwa na mlipuko wa moto uliotokea kiwandani hapo jana Septemba 24, 2021, baada ya kinu cha uji wa moto kulipuka ambapo waliokuwa karibu ndiyo walioathiriwa zaidi na joto la uji wa vyuma.

Majeruhi hao walifikishwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, na kupokelewa na daktari wa magonjwa ya jumla wa hospitali hiyo Dkt. Diana Anatory, ambapo amesema baadhi yao walikuwa wanalalamika kuwa na shida ya upumuaji pamoja na kuwa na majeraha ya mwilini.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mwanza, Ambwene Mwakibete, alisema mlipuko huo wa joto la uji wa vyuma umewaathiri wafanyakazi waliokuwa eneo hilo na wengine waliokua mbali wameathirika kwa kurukiwa na uji huo na amewataka wamiliki wote wa viwanda kuchukua tahadhari kwa wafanyakazi wao kwa kuhakikisha wanavaa vifaa vya usalama na kujikinga na madhara ya moto.

Aidha kwa mujibu wa taarifa ya daktari majeruhi 33 waliruhusiwa kurudi nyumbani na majeruhi saba walilazwa.

Chanzo - EATV

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post