Breaking

Post Top Ad

https://refpasrasw.world/L?tag=d_1066073m_7669c_&site=1066073&ad=7669

Saturday, September 25, 2021

JAMAA ACHOMA NYUMBA YA MWANAMKE ALIYEMHONGA POMBE AKABEBWA NA MWANAUME MWINGINEKatika hali ya kusikitisha, mwanamke aitwaye Felista Michael mkazi wa kijiji cha Wama, Kata ya Gisambala wilayani Hanang Mkoani Manyara amenusirika kifo mara baada ya kuchomewa nyumba yake na mtu aliyefahamika kwa majina ya Heriko Selastin huku kisa kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Merisone Mwakyoma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kwamba Heriko alimnunulia pombe mpenzi wake Felista kwa makubaliano ya kuondoka naye lakini baadaye mwanamke huyo aliondoka na mwanaume mwingine ambaye naye alielezwa kumnunulia pombe pia, jambo ambalo lilimtia hasira Heriko na kuamua kwenda kuichoma nyumba ya mpenzi wake huyo.

Katika tukio jingine, mtu mmoja anayefahamika kwa majina ya Isaka Yustin mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa kijiji cha Emango kilichopo Kata ya Galapo wilaya ya Babati Mkoani Manyara ameuawa na aliyekuwa mkewe kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali shingoni.Jeshi la Polisi mkoani Manyara bado linaendelea na uchunguzi kufuatia matukio hayo ya kinyama.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages