WACHIMBAJI WATAKIWA KUKATA LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI GEITA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Saturday, September 18, 2021

WACHIMBAJI WATAKIWA KUKATA LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI GEITA


Mtakwimu wa tume ya madini Azihar Kashakara akieleza utendaji kazi na maboresho ya tume hiyo kwa kamati ya siasa ilipotembelea kwenye banda hilo. Picha zote na Alphonce Kabilondo
Mwenyekiti wa Chama Cha wachimbaji wadogo mkoa wa Geita Christopher Kadeo akitoa maelezo mbele ya kamati ya siasa ilipotembelea kwenye banda hilo.
Kamati ya siasa ikipata maelezo kutoka kwa afisa masoko mwandamizi wa mfuko wa bima ya afya (NHIF) Flora Mataba


Na Alphonce Kabilondo,Geita

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Geita mkoani Geita imewataka wachimbaji wadogo kukata leseni za uchimbaji katika maeneo yao ili kuondoa migogoro pindi yanapoibuka madini ya dhahabu.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Barnabas Mhoja Mapande ametoa kauli hiyo leo alipotembelea mabanda ya maonesho ya nne ya teknolojia ya uchimbaji madini yanayoanyika eneo la EPZ mjini Geita.

Mapande amesema kuwa hao wachimbaji wadogo hawana budi kufika ofisi ya tume madini kuomba leseni ya uchimbaji ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea pindi madini yanapoibuka kwenye maeneo yao.

Aidha kamati hiyo ikiwa kwenye banda la tume ya madini imetumia fursa hiyo kuipongeza tume ya madini kwa kuboresha utoaji wa leseni kwa kutuma maombi kwa njia ya mtandao.

“Nitumie fursa hii kuwaomba wananchi wachimbaji wadogo wa madini kujitokeza kwenye maonesho haya kuona na kujiunza teknolojia ya uchimbaji wa kisasa”, alisema Mwenyekiti.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji wa Madini Mkoani Geita (GEREMA) Christopher Kadeo ameiambia kamati hiyo kuwa baadhi ya wachimbaji wameingiwa na sintofahamu baada serikali ya kuwapa notisi za kukusudia kuwafutia leseni zao.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages