KATAMBI ATOA MSAADA WA COMPUTER, PRINTER SHULE ZA SEKONDARI NGOKOLO NA CHAMAGUHA


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Patrobasi Katambi, kushoto, akimkabidhi Kompyuta Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Sawaka, kati ya Kompyuta tano na Printer moja ambazo ametoa shuleni hapo.


Na Marco Maduhu, Shinyanga

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ametoa vitabu vya Sayansi na Kompyuta kwa shule za Sekondari Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza leo wakati wa kubidhi vitabu hivyo na Kopyuta, akiwa katika Shule ya Sekondari Chamaguha na Ngokolo, amesema ametoa vifaa hivyo vya masomo ili kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi.

Amesema kipindi cha Kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2020, aliahidi kutatua changamoto mbalimbali katika jimbo hilo la Shinyanga Mjini, ikiwemo Sekta ya Afya, miundombinu ya barabara pamoja na Elimu, ambapo kwa sasa ameanza utekelezaji wa ahadi zake kwa kila sekta, na kutoa vifaa hivyo vya masomo ya Sayansi.

“Kipindi cha kampeni tulikuwa tunaahidi, na sasa tunatekeleza yale yote tuiyokuwa tukinadi kwenye ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi CCM yenye kurasa 303, na tutatekeleza ahadi zote kwa wananchi,”alisema Katambi.

“Nimetoa vitabu vya masomo ya Sayansi 324 na vitabu vya miongozi ya walimu, kwa shule za Sekondari Nne za Manispaa ya Shinyanga, ambazo ni Chamaguha, Oldshinyanga, Mwamalili na Ibadakuli, vitabu 81 kwa kila shule, na katika shule hii ya Sekondari Ngokolo ninatoa Kompyuta tano, na Printer moja,”aliongeza.

Aidha alisema ametoa vitabu hivyo, ili kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi, na kuiona Shinyanga inapata wataalam wake wa baadaye na kuwaletea maendeleo, huku akiwataka wanafunzi wajikite kwenye masomo, yao na kuacha kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na ngono katika umri mdogo.

Naye, Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Sawaka, na Mkuu wa Shule ya Sekondari Chamaguha Mwesa Martini, kwa nyakati tofauti walimpongeza Mbunge huyo kwa kuwapatia vitabu hivyo pamoja na Kompyuta, vifaa ambavyo zitachochea ukuaji wa elimu na kufaulisha wanafunzi wengi wa masomo ya Sayansi.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Patrobas Katambi, akizungumza kwenye hafla ya kugawa Kompyuta katika Shule ya Sekondari Ngokolo na kueleza kuwa anatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune, akizungumza kwenye zoezi la Katambi la kukabidhi Vitabu na Kompyuta kwa shule za Sekondari Manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa Ngokolo Victor Mkwizu, akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya Kompyuta katika shule ya Sekondari Ngokolo kutoka kwa Mbunge Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Sawaka, akishukuru kupewa Kompyuta hizo.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Chamaguha Mwesa Martini, akishukuru kupewa vitabu 81 vya Masomo ya Sayansi.

Katambi, mkono wa kulia ,akikabidhi Vitabu 81 vya Masomo ya Sayansi kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Chamaguha Mwesa Martini.

Katambi, kushoto, akikabidhi Kompyuta kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo Malale Sawaka.

Katambi, akikabidhi Printer kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Ngokolo.

Katambi akipiga picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo, huku wakishikilia Kopyuta, kulia ni Diwani wa Ngokolo Victor Mkwizu.

Katambi akiwasihi Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo, kusoma kwa bidii na kutojiingiza kwenye Madawa ya Kulevya na Mapenzi katika umri mdogo bali wasome ili watimize malengo yao.

Awali Katambi, akijionea na kusikiliza namna wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo Jinsi wanavyosoma Masomo ya Sayansi kwa vitendo.

Masomo ya Sayansi kwa vitendo yakiendelea.

Katambi akipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngokolo, ambao walifanya vizuri kwenye mashindano ya masomo ya Sayansi na kubeba Tuzo, yaliyofanyika katika shule ya Savanna mwaka huu.

Awali vijana wa Skauti katika Shule ya Sekondari Ngokolo, wakimvalisha Katambi Skafu, alipowasili Shuleni hapo kukabidhi Kopyuta tano na Printer moja.

Na Marco Maduhu- Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post