GEITA GOLD FC KUTUMIA CCM KAMBARAGE UWANJA WA NYUMBANI...KESHO WATAKIPIGA NA SHINYANGA COMBINE | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 1, 2021

GEITA GOLD FC KUTUMIA CCM KAMBARAGE UWANJA WA NYUMBANI...KESHO WATAKIPIGA NA SHINYANGA COMBINE

  Malunde       Wednesday, September 1, 2021

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Timu ya Geita Gold FC inatarajia kutumia uwanja wa CCM Kambarage kama uwanja wa nyumbani Ligi Kuu Soka Tanzania bara msimu wa 2021/2022 ambapo kesho Septemba 2, 2021 itacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Shinyanga Combine.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga, Said Mankiligo amesema tayari Kocha Mkuu Ndairagije aliyekuwa Kocha Mkuu wa Taifa Star na Msaidizi wake Fred Felix Minziro na kikosi chote cha timu wameshawasili Mjini Shinyanga.

“Timu ya Geita Gold Football Club imechagua uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini kuwa uwanja wa nyumbani kwa kipindi hiki ambacho wanaendelea na matengenezo ya uwanja wao”,amesema Mankiligo.

“Timu ya Geita imewasili Shinyanga tangu Agosti 31,2021 na leo wameanza rasmi mazoezi yao na kesho Alhamis saa 10 jioni watacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Shinyanga Combine (inayojumuisha Mastaa wote Shinyanga) katika uwanja wa CCM Kambarage”,ameongeza Mankiligo.

Amesema pia Timu ya Geita Gold FC inatarajia kucheza michezo ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara (Pre Season) na timu za Police Tanzania na Biashara United ya mkoani Mara ambapo ratiba ya michezo itatangazwa kesho.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post