Breaking

Post Top Ad

https://refpasrasw.world/L?tag=d_1066073m_7669c_&site=1066073&ad=7669

Monday, August 16, 2021

WABUNGE SASA KUANZA KUFANYIWA 'MASSAGE' BUNGENI KUONDOA UCHOVU WANAPOTUNGA SHERIAWabunge nchini Kenya wanatazamiwa kuanza kupata huduma za ukandaji 'Massage' katika majengo ya bunge iwapo ripoti iliyowasilishwa na kamati ya Huduma za Vifaa Hitajika Bungeni itapitishwa.

Kamati hiyo ilisema pendekezo hilo ni kwa minajili ya kuimarisha afya ya wabunge kutokana na kukabiliwa na wakati mgumu wanapotunga sheria. 

Kando na hayo, pia inataka kituo cha afya bungeni kikarabatiwe kulingana na sheria za Wizara ya Afya za kuzuia msambao wa corona.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Nyaribari Masaba, Ezekiel Machogu ilisema kituo hicho pia kinatakiwa kipanuliwe ili kuongeza vyumba vya ukandaji, kinyozi na ususi. 

"Kitengo cha wanaume kipanuliwe ili kiwe na vyumba vya kutoa ulimwende na mazoezi ya viungo," ilisoma ripoti hiyo.

Kamati hiyo pia inataka kitengo cha wanawake kiwe na huduma za kurembesha kucha na kutengeneza nywele.

 Wafanyakazi wa kituo hicho cha afya watapewa kandarasi ya miaka mitano yenye uwezekano wa kurefusha kulingana na utendakazi iwapo ripot hiyo itapitishwa.

 Chanzo - Tuko News

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages