TATIZO LA MTANDAO LAKWAMISHA KESI YA MBOWE, YAAHIRISHWA MPAKA KESHO | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, August 5, 2021

TATIZO LA MTANDAO LAKWAMISHA KESI YA MBOWE, YAAHIRISHWA MPAKA KESHO

  Malunde       Thursday, August 5, 2021

Kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, imeahirishwa hadi kesho Agosti 6, 2021, kutokana na muonekano hafifu wa video conference, kesi hiyo ilikuwa inaendeshwa kwa mfumo huo, ambapo kesho atafikishwa mahakamani majira ya saa 3:00 asubuhi.


Kesi hiyo ya ugaidi ilikuwa itajwe leo Agosti 5, 2021, ambapo Mbowe na wenzake walikuwa katika Gereza la Ukonga Dar es Salaam lakini kutokana na matatizo ya mtandao ilishindwa kuendeshwa vizuri.

Akizungumza hii leo mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala, amesema kuwa, "Teknolojia imefeli hivyo tumeshindwa kufanikisha mchakato huo kwa sababu kumekuwa na mawasiliano hafifu kati ya video conference facility za hapa katika Mahakama ya Kisutu na Gereza la Ukonga na tumekubaliana kwamba kesho washtakiwa waletwe mahakamani".


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post