SAVE THE CHILDREN, WADAU WACHAMBUA BAJETI MANISPAA YA SHINYANGA SEKTA ZINAZOHUSU WATOTO...NAIBU MEYA APONGEZA

Naibu Meya Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akizungumza wakati akifunga Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Meya Manispaa ya Shinyanga Ester Makune amefunga Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children kikiwa na lengo la kuangalia jinsi gani halmashauri imetenga fedha za kutosha kuhusu mambo yanayogusa watoto.

Akifunga kikao hicho kilichofanyika kwa muda wa siku mbili leo Ijumaa Agosti 20,2021, Mhe. Makune amelipongeza shirika la Save The Children kwa kukutanisha wadau wakiwemo watumishi wa serikali (maafisa bajeti) Manispaa ya Shinyanga, Wataalamu kutoka ngazi ya Mkoa wa Shinyanga, Wawakilishi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na asasi za Kiraia zinazotekeleza miradi katika masuala ya watoto.

Mhe. Makune amesema kikao hicho kimekuwa na manufaa makubwa kwani wadau wameweza kuchambua Bajeti ya Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto hali ambayo itachochea kuleta mabadiliko katika bajeti zijazo ili iwaguse watoto moja kwa moja huku akisisitiza umuhimu wa kila mmoja katika jamii kuwajali na kuwalinda watoto.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Shinyanga Bi. Octavina Kiwone amezishukuru taasisi na mashirika yote yakiongozwa na Save The Children kwa namna wanavyogusa maisha ya watoto na kuchangia katika shughuli mbalimbali za maendeleo

“Pia tunaishukuru serikali kuu kwa kuwezesha halmashauri yetu kifedha hivyo kuwezesha utekelezaji wa bajeti zetu lakini pia wananchi kwa kuendelea kuunga mkono shughuli zinazofanywa na serikali”,amesema Octavina.

Akizungumza kwa niaba ya Asasi za Kiraia zilizoshiriki kikao hicho, Mkurugenzi wa Shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng’ong’a amelipongeza shirika la Save The Children kwa kazi nzuri linalozifanya kwa kushirikiana na wadau na serikali katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii hususani kwa watoto.

Kwa upande wake, Mtaalamu wa Utekelezaji wa Haki za Watoto wa Shirika la Save The Children, Wilbert Muchunguzi amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na wadau na serikali katika kupigania masuala yanayohusu watoto hivyo kuomba ushirikiano zaidi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Mratibu wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Kiuchumi na Utawala wa Fedha kutoka Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga, Alex Enock amesema kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo wenye lengo la kuimarisha Mijadala na kuongeza mijadala katika masuala ya uchumi na Utawala wa Fedha, unaotekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga na Shirika la Save The Children na Uratibu wa Wizara ya Fedha kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya.

Miongoni mwa changamoto zilizoibuka kwenye kikao hicho ni pamoja na Bajeti ndogo zinazotengwa kwa ajili ya masuala yanayogusa watoto hivyo wameshauri ni vyema kuongeza bajeti na kuwa na vipaumbele vichache vinavyohusu watoto badala ya kujikita kwenye kuboresha miundo mbinu tu bila kuangalia vitu vingine vinavyomgusa mtoto moja kwa moja yakiwemo mahitaji ya taulo laini ‘Pedi’.

Washiriki hao wa kikao pia wameshauri Mchakato wa bajeti uwe jumuishi kwa kushirikisha makundi mbalimbali katika jamii ili bajeti iwe na majibu ya mahitaji ya wananchi.

Aidha wamebaini kuwa mahitaji yanayogusa ulinzi wa motto hayajaainishwa moja kwa moja hivyo ni vyema Halmashauri ya idadavue fedha zinazotolewa zinaenda kunufaisha maeneo yapi.

Pia wamesema bado masuala ya ulinzi wa mtoto hayajapewa rasilimali za kutosha katika utekelezaji wake hivyo kushindwa kuwekeza vya kutosha kuhusu watoto.

Hali kadhalika wameshauri kuwe na muungano wa ajenda Kikanda,Kimkoa na taifa kuhusu masuala yanayohusu watoto na kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya bajeti watumishi wa halmashauri wa idara zinazohusu bajeti.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Naibu Meya Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akizungumza leo Ijumaa Agosti 20,2021 wakati akifunga Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Meya Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akizungumza wakati akifunga Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children. Kushoto ni Mtaalamu wa Utekelezaji wa Haki za Watoto wa Shirika la Save The Children, Wilbert Muchunguzi, kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng’ong’a.
Mtaalamu wa Utekelezaji wa Haki za Watoto wa Shirika la Save The Children, Wilbert Muchunguzi akizungumza wakati wa ufungaji wa Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Mkurugenzi wa Shirika la Rafiki SDO, Gelard Ng’ong’a akizungumza wakati wa ufungaji wa Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Mratibu wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Kiuchumi na Utawala wa Fedha kutoka Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga, Alex Enock  akizungumza wakati wa ufungaji wa Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Shinyanga Bi. Octavina Kiwone akizungumza wakati wa Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Edson Toto akizungumza wakati wa Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Abel Sengasenga akizungumza wakati wa Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Mwezeshaji wa kikao hicho, Geofrey Chambua  akiangalia mapendekezo ya masuala ya bajeti kwa kila mshiriki kwenye Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Mwezeshaji wa kikao hicho, Geofrey Chambua  akiangalia mapendekezo ya masuala ya bajeti kwa kila mshiriki kwenye Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Washiriki wa kikao hicho wakijadili jambo kwenye Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Washiriki wa kikao wakiandika mapendekezo yao kuhusu masuala ya bajeti kwa kila mshiriki kwenye Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Washiriki wa kikao wakiandika mapendekezo yao kuhusu masuala ya bajeti kwa kila mshiriki kwenye Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children wakipiga picha ya kumbukumbu
Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children wakipiga picha ya kumbukumbu.

 Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post