SAVE THE CHILDREN YAKUTANA NA WADAU KUCHAMBUA BAJETI SEKTA ZINAZOGUSA WATOTO MANISPAA YA SHINYANGA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Thursday, August 19, 2021

SAVE THE CHILDREN YAKUTANA NA WADAU KUCHAMBUA BAJETI SEKTA ZINAZOGUSA WATOTO MANISPAA YA SHINYANGA

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akifungua Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Save The Children limeendesha Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ambazo ni Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa Mtoto kwa lengo la kuangalia jinsi gani halmashauri zimetenga fedha za kutosha kuhusu mambo yanayogusa watoto.

Kikao Kazi hicho cha siku mbili kimefunguliwa leo Alhamisi Agosti 19,2021 katika ukumbi wa Vigirmark Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha watumishi wa serikali (maafisa bajeti) Manispaa ya Shinyanga, Wataalamu kutoka ngazi ya Mkoa wa Shinyanga, Wawakilishi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na asasi za Kiraia zinazotekeleza miradi katika masuala ya watoto.

Akifungua Kikao hicho kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, John Tesha amelipongeza shirika la Save The Children kwa kuandaa kikao hicho huku akiwataka wanajamii wote kushiriki katika kulinda watoto.

“Nishukuru sana Save The Children wamekuwa karibu sana na serikali na wanafanya kazi nzuri. Nawapongeza kwa sababu sekta wanazohusika nazo kuhusu mtoto ni muhimu", amesema.

“Kipengele cha bajeti hasa bajeti ya kusaidia watoto limekuwa mjadala mkubwa na sasa unaendelea vizuri ili kuhakikisha watoto wanapata haki wanazostahili. Kuhusu Mijadala ya Jumuishi katika masuala ya fedha naomba kila mtu atoe maoni yake namna gani tunaboresha bajeti zetu”,ameeleza Tesha.

Mashirika yasiyo ya kiserikali kuungana pamoja na kuhakikisha wanasaidia serikali katika kulinda haki za watoto huku akibainisha kuwa familia ndiyo msingi mzuri wa malezi ya mtoto hivyo lazima anapaswa kuwajibika kulinda haki za watoto na kuona kuwa kila mtoto anayemuona ni wake.

Mratibu wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Kiuchumi na Utawala wa Fedha kutoka Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga, Alex Enock amesema Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga na Shirika la Save The Children na Uratibu wa Wizara ya Fedha kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya.

“Lengo la Mradi huu ni kuimarisha Mijadala na kuongeza mijadala katika masuala ya uchumi na Utawala wa Fedha. Katika Kikao kazi hiki tutaangalia kwa jinsi gani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imetenga fedha kuhusu mambo yanayogusa watoto katika sekta za Afya, Elimu, Lishe na Ulinzi wa mtoto”,amesema Enock.

“Kikao hiki pia kimelenga kujenga uwezo kwa wadau wa masuala ya watoto katika kuchambua bajeti na uelewa katika masuala ya bajeti na utekelezaji wa haki za watoto”,ameeleza.

Ameongeza kuwa katika kikao hicho pia watatengeneza Muhtasari wa Bajeti ambao utatoa taarifa na mrejesho wa hali halisi ya utengaji bajeti ya mtoto sambamba na kutengeneza mbinu za kuelezea changamoto na mapendekezo katika ngazi mbalimbali ili kufanyiwa kazi.

Kwa upande wake, Mtaalamu wa Utekelezaji wa Haki za Watoto wa Shirika la Save The Children, Wilbert Muchunguzi amesema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha analinda haki za watoto.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akifungua Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children. Kushoto ni Mtaalamu wa Utekelezaji wa Haki za Watoto wa Shirika la Save The Children, Wilbert Muchunguzi.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akifungua Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akifungua Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Mtaalamu wa Utekelezaji wa Haki za Watoto wa Shirika la Save The Children, Wilbert Muchunguzi akizungumza katika Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Mratibu wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Kiuchumi na Utawala wa Fedha kutoka Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga, Alex Enock akielezea lengo la Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.
Mratibu wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Kiuchumi na Utawala wa Fedha kutoka Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga, Alex Enock akizungumza katika Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children.

Washiriki wa  Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti Manispaa ya Shinyanga katika Sekta zinazohusu Watoto kilichoandaliwa na Shirika la Save The Children wakiwa ukumbini.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages