MKUTANO WA NNE WA TUME YA PAMOJA YA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA KENYA WAFANYIKA NAIROBI, KENYA.




Balozi Naimi S.H. Azizi Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya uliokuwa ukiendela katika Hoteli ya Movenpick Jijini Nairobi, Kenya.

Balozi Naimi S.H. Azizi Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya unofanyika Jijini Nairobi Kenya

Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Mhe. Dkt. John Simbachawene akifuatilia Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya uliokuwa ukiendela katika Hoteli ya Movenpic Jijini Nairobi, Kenya.

Sehemu ya Wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya uliokuwa ukiendela katika Hoteli ya Movenpick Jijini Nairobi, Kenya

Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya ukiendelea.

Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya unaendelea Jijini Nairobi, Kenya wakiwa katika picha ya pamoja.

Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya ukiendelea.

Mhe. Ababu Namwamba, Katibu Mkuu wa Utawala katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya unofanyika Jijini Nairobi Kenya

*************************

Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya umeanza kufanyika leo tarehe 19 Agosti 2021 Jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huu utakaofanyika kwa kipindi cha siku sita kuanzia tarehe 19 hadi 24 Agosti, 2021 unalenga kujadili mambo mbalimbali muhimu ya ushirikiano ikiwemo Mahusiano ya Kidiplomasia, Ulinzi na Utawala Bora, Uchumi na Biashara, na Masuala ya Kijamii sambamba na kuibua maeneo mapya ya ushikiano kwa lengo la kuchagiza maendeleo baina ya Tanzania na Kenya. 

 

Mkutano huu muhimu katika ustawi wa ushirikiano na maendeleo baina ya mataifa haya mawili, unafanyika ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ziara yake aliyoifanya Nchini Kenya mwezi Mei, 2021, kuwa Nchi hizi mbili zifanye Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano.  

 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano huo katika ngazi ya Wataalamu, Balozi Naimi S.H. Azizi, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amebainisha kuwa mkutano huo umetoa fursa hadhimu kwa pande zote mbili kukutana ili kuweka mipango na mikakati ya pamoja itakayoimarisha ushirikiano kwenye utekelezaji wa vipaumbele vya shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali kwa manufaa ya pande zote mbili.

“Natambua vyema kuwa tokea Mkutano wa Mwisho wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano ulipofanyika, mengi mazuri yamefanyika baina ya Nchi zetu (Tanzania na Kenya) na kwa kupitia miogozo ya Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mathalani nilifarijka sana pale timu yetu ya Wataalamu ya Pamoja ya kudhibiti Mipaka ilipofanya Mkutano wao kwa mafanikio Juni 2021, Jijini Mombasa, Kenya. Hili linaendelea kudhihirisha utayari wa Serikali zetu wa kudumisha amani na kuleta maendeleo”. Alisema Balozi Naimi S.H. Azizi.  
 
Balozi Naimi S.H. Azizi aliongeza kusema kuwa ni muhimu wajumbe wa mkutano wajikite katika kujadili masuala muhimu yenye maslahi kwa pande zote mbili ili kukidhi matarajio ya Wakuu wa Nchi hizi mbili, ya kuona Wataalamu katika Serikali wanazoziongoza wanaendelea kuwajibika ipasavyo katika kuwaletea maendeleo wananchi. 
 
Mkutano huu umejumuisha Viongozi, Watendaji na Maafisa mbalimbali wa Serikali kutoka Tanzania na Kenya. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments