SABAYA ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI, KESI YAAHIRISHWA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo imeahirisha usikillizaji wa ushahidi wa shahidi namba saba upande wa Jamhuri wa kesi ya jinai  namba 105 ya mwaka 2021 ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili  kutokana na Mshtakiwa namba Moja Ole Sabaya  kutokufika mahakamani kutokana na sababu za kiafya.

Akiahirisha shauri Hilo Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo amesema shauri hilo litaendelea kesho Agosti 05 asubuhi kwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa shahidi namba saba Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Gwakisa Minga ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai wilaya ya Arusha.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments