RAIS SAMIA AAGANA NA RAIS KAGAME RWANDA..AREJEA TANZANIA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, August 3, 2021

RAIS SAMIA AAGANA NA RAIS KAGAME RWANDA..AREJEA TANZANIA

  Malunde       Tuesday, August 3, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rwanda baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Nchini Rwanda leo tarehe  03 Agosti,2021. Picha na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia moja ya aina ya simu zinazotengenezwa katika kiwanda cha Mara Phone Mjini Kigali Rwanda, wakati alipokua katika ziara yake ya siku ya pili nchini Rwanda leo tarehe 03 Agosti,2021. Kulia ni Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana  na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame mara baada ya kuwasili katika eneo la Uwekezaji wa kiwanda cha Inyange Plant Entrance kilichopo mjini Kigali Rwanda leo Agosti 03,2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda wakitembelea katika kiwanda cha Inyange Plant Entrance mjini Kigali kinachozalisha Juisi, Maziwa na Maji ya kunywa leo tarehe 03 Agosti,2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenyeji wake Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakiangalia baadhi ya Bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika kiwanda cha Inyange Plant Entrance mjini Kigali wakati walipotembelea kiwanda hicho leo tarehe  03 Agosti,2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, wakiwa katika picha mbele ya Gari aina ya Volkswagen mara baada ya kutembelea kwenye Kiwanda cha kutengenezea Magari CFAO MOTORS Mjini Kigali Nchini Rwanda leo tarehe  03 Agosti,2021.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post