NG’OMBE 6270 WATAMBULIWA KWA KUVISHWA HERENI KATIKA KIJIJI CHA KITOSI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, August 14, 2021

NG’OMBE 6270 WATAMBULIWA KWA KUVISHWA HERENI KATIKA KIJIJI CHA KITOSI

  TANGA RAHA BLOG       Saturday, August 14, 2021


Ng'ombe 6270 wametambuliwa kwa njia ya Kuvishwa Hereni za kielektroniki katika kijiji cha Kitosi Wilayani,Nkasi Mkoa wa Rukwa.

Haya yamebainishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kwenye, Mkutano na wafugaji katika Kijiji cha Kitosi mara baada ya kushiriki katika zoezi la uwekeji herenikatika kijiji hicho.

Waziri Mashimba amesema kuwa zoezi la utambuaji wa Mifugo linatekelezwa nchini kote na kwa sasa tumeanza na mikoa ya Mfano ambayo ni Rukwa ,Katavi , na Kigoma.

Amesema zoezi hili limeanza Katika kijiji cha Kitosi Wilaya ya Nkasi na tangu zoezi hili limeanza zaidi ya ng'ombe 6270 tayari wameisha tambuliwa kwa kuvishwa hereni katika kiji hicho.

Amesema zoezi hili nimuhimu kwa kuwa linaongeza thamani ya Mifugo ya wafugaji katika Masoko na kusaidia kufuatilia ubora wa mazao yanayo zalishwa na Mifugo iliyotambuliwa kwa njia ya hereni.

Amefafanua kuwa Mifugo itakayozalishwa itakidhi mahitaji ya soko la nje la Mifugo yetu na mazao yake.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post