MAKUNDI LIGI YA MABINGWA ULAYA YAPANGWA, PSG KUKUTANA NA MACHESTER CITY


**************************

NA EMMANUEL MBATILO

Baada ya kushuhudia droo ya Klabu bingwa Ulaya ikipangwa leo tumeona kundi A likiwa limejaa wababe ambapo kuna timu ya PSG,Manchester City, RB Leipzig na Club Brugge hivyo tutatazama miamba miwili kati ya PSG na Manchester City wakiumana kwenye kundi hilo.

Ikumbukwe yakuwa kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Ureno Christian Ronaldo kujiunga na Manchester City kwenye majira haya ya usajili.

Mabingwa wa Ulaya waliopita Chelsea wao wamepangwa kwenye kundi H ambapo amepangwa na klabu ya Juventus, Malmo na Zenit St. Petersburg.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments