KISUVITA WAJA NA MASHINDANO YA UREMBO WA VIZIWI | MALUNDE 1 BLOG

Monday, August 9, 2021

KISUVITA WAJA NA MASHINDANO YA UREMBO WA VIZIWI

  Malunde       Monday, August 9, 2021

Adeladius Makwega, WHUSM –Dodoma
SERIKALI imekipongeza Kituo cha Sanaa na Utamaduni kwa Viziwi Tanzania (KISUVITA) kwa kuanzisha mashindano ya Miss&Mister Deaf Tanzania ambayo yanayotarajiwa kufanyika septemba 2021.

Akizungumza Ofisini kwake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mfaume Said amesema kuwa mashindano haya washindi watakaopatikana watashiriki katika mashindano Kimataifa ya viziwi.

“Kuna vijana na warembo wengi wenye sifa zote kwa ndugu zetu viziwi, hili ni jambo jema na wizara tukishirikiana na KISUVITA maandalizi ya msingi yamekamilika.”Alisema Kaimu Mkurugenzi huyo.

Serikali imetoa na itaendelea kutoa ushirikiano wote kwa KISUVITA kwani wanalolifanya ni jambo la Watanzania na wizara yetu ndiye msimamizi mkuu wa masuala yote ya sanaa.

Akitoa maelezo ya mashindano hayo Bi. Hadija Kisubi ambaye ni Afisa Utamaduni wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo amesema kuwa haijawahi kutokea mashindano makubwa kama haya ambapo yatakuwa ya kukata na shoka.

“Kama alivyozungumza Kaimu Mkurugenzi wetu Sanaa, mashindano haya yanatarajiwa kufanyika Septemba 14, 2021 katika ukumbi wa Serana Mkoani Dar es Salaam.”

Akizungumzia mashindano hayo Habibi Mrope ambaye ni Mkurugenzi wa KISUVITA amesema kuwa hapo awali waliomba msaada kutoka kwa wadau wengine lakini zoezi hilo liligonga mwamba.

“Lakini tulipowasiliana na wizara yetu jambo hili limekuwa jepesi na limeungwa mkono kwa asilimia 100 na sasa sisi kama KISUVITA tunatembea kifua mbele na hatua za mwisho za kukamilisha mashindano haya zimeshafikiwa. Nawaomba Watanzania mjitokeze kufuatilia mashindano hayo.” Alisema Mkurugenzi huyo wa KISUVITA.

Washindi wanne watakaopatikana katika mshindano hayo wataiwakilisha nchii katika mashindano ya Afrika na baadaye ya Dunia yatakayofanyika mwezi wanne mwakani huko Brazili.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post