JAMAA ATIWA MBARONI KWA KUMDUNGA KISU MARA 17 MKEWE WALIYEACHANA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, August 15, 2021

JAMAA ATIWA MBARONI KWA KUMDUNGA KISU MARA 17 MKEWE WALIYEACHANA

  Malunde       Sunday, August 15, 2021


Mwanaume mmoja amekamatwa kwa kumdunga kisu mkewe waliyeachana mara 17 kulingana na simulizi ya mwanao na majirani waliofika eneo la tukio.

  Mtoto huyo alitoa maelezo muhimu kwa polisi amnbayo huenda yanaweza kusaidia kutatua kitendawili cha mauaji ya Esther Nyaga, muuguzi katika Zahanati ya Muruka Kandara, Kaunti ya Murang'a nchini Kenya.

 Iliripotiwa kuwa wapenzi hao walikuwa katika harakati za kutalikiana na Evans Njacha Kamau alikuwa ameamriwa na mahakama kutozuru boma lao.

Kulingana na familia, Esther alikuwa ameripoti kushambuliwa mara kwa mara na mumewe ambaye walikuwa wametengana lakini polisi walimpuuza tu.

 Kamau na Esther walioana mnamo 2010 lakini walitengana mnamo 2019. Wana watoto watatu (binti wa miaka 11 na wana wa kiume wa miaka 7 na 2).

Siku ya mauaji yake ya kikatili, jamaa zake walidai kwamba mtuhumiwa aliingia nyumbani na kuzima umeme.

 Mjakazi alimwona mtu aliyekuwa amejihami kwa kisu na bastola naye akaanza kukimbilia usalama wake akipiga mayowe. 

Esther alielekea jikoni baada ya kusikia vurugu kabla ya mshambuliaji kumtokea ghafla na kumuamuru kumpa pesa kabla ya kumuamuru kuelekea naye katika chumba cha kulala. 

Walipofika katika chumba chake cha kulala, mshukiwa alianza kumdunga kisu. 

Mshukiwa huyo aliondoka chumbani humo kumtafuta mjakazi ambaye alikuwa amejificha na ndiposa wakati huo watoto waliitambua sauti yake. 

Baadaye mshukiwa alihepa. Esther aliwaita watoto wake na kuwaambia wamjulishe jirani yao ili aje ampeleke hospitalini.

 Wakiwa njiani, Esther aliwaambia kuwa mumewe ndiye mshukiwa mkuu aliyemshambulia. 

Ripoti ya uchunguzi wa baada ya kifo ilionyesha kuwa muuguzi huyo alikuwa na majeraha mabaya tumboni na mshukiwa pia alijaribu kumchinja. 

Uchunguzi wa mauaji hayo bado unaendelea na mtuhumiwa atarudishwa kortini Jumatano, Agosti 18,2021.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post