Breaking

Post Top Ad

https://refpasrasw.world/L?tag=d_1066073m_7669c_&site=1066073&ad=7669

Sunday, August 8, 2021

SAUDIA YAFUNGUA MIPAKA KWA MAHUJAJI WALIOCHANJWA CHANJO YA CORONASAUDIA ARABIA itaanza kuwapokea wageni waliopata chanjo ya Covid-19 katika mji mtukufu wa Kiislamu wa Makka ikiwa kama sehemu ya ibada ya umrah, ni takriban miezi 18 tangu kuifunga mipaka yake baada ya kuzuka janga la virusi vya corona.

Shirika la habari la Saudia limesema Wizara ya Hijja na Umrah imetangaza kuanzia kesho Jumatatu watapokea maombi ya raia na wakazi wake wanaotaka kushiriki ibada ya Umrah.

Lakini pia baadaye watapokea maombi kutoka mataifa mbalimbali ya nje, ruhusa hiyo hata hivyo imetolewa kwa masharti kwamba mahujaji wote wa kigeni lazima wawe wamepata chanjo inayotambuliwa na Saudi Arabia na wakubali kukaa karantini.

Ibada ya Umrah ambayo kwa kawaida inafanyika katika kipindi chochote cha mwaka, ilifunguliwa tena Oktoba kwa mahujaji wa ndani, baada ya kufungwa kabisa kutokana na mlipuko wa janga la virusi vya corona.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages