WCF YATOA TAMKO LA PUNGUZO LA TOZO KWA WAAJIRI WA SEKTA BINAFSI
Na Dickson Billikwija, Dar es Salaam

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umesema waajiri wa Sekta Tanzania  wamepunguziwa kiwango cha mchango wa wafanyakazi cha mapato ya waajiriwa wao kutoka asilimia 1 hadi asilimia 0.6 huku ukibainisha punguzo la kiwango hicho linaanza kutumika kwa michango ya mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo, Dkt. John Mduma amesema mabadiliko ya punguzo hilo yamekuja baada ya Bunge la Bajeti la mwaka 2021/22 kuweka bayana ya upunguzaji wa tozo ikiwa utekelezaji wa Blueprint na kwamba madiliko hayo yapo kwa mujibu wa Tangazo la Serikali  namba 496G la juni 30 mwaka huu lililotolewa dhamana na waziri husika Jenista Mhagama.

Amebainisha kuwa  licha ya punguzo la tozo la uchangiaji katika mfuko huo waajiriwa wa sekta binafsi  wataendelea mafao ya fidia kama ilivyokuwa awali kwa mujibu wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi na kanuni zake za mwaka 2016.

Amesisitiza kuwa punguzo hilo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inayoelekeza mfuko kuboresha mazingira ya biashara na ufanyaji kazi wa sekta binafsi jkwa kuiwekea mazingira rafiki.

Ameongeza kuwa  punguzo hilo litakuwa na mchango mkubwa kwa sekta hiyo ikiwemo kupunguza gharama za uendeshaji za waajiri, kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini na  kuboresha na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya waajiri na WCF.

Amekipongeza Chama cha Waajiri nchini (ATE)  kwa mchango mkubwa katika  uboreshaji wa huduma  za waajiri na kushughulikia  masuala ya mbalimbali yahayohusu waajiri na waajiriwa likiwemo suala la tozo huku 

Dkt. Mduma amesema WCF inamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi ya kupunguza  tozo kwa waajiri wa sekta binafsi  na kulipongeza Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kuwa mstari mbele kuhakikisha waajiri wanafanya kazi wakiwa na uhakika wa kingaz za mwili.

Aidha, amesema mfuko huo una thamani ya Sh Bilioni 437 na kwamba katika kipindi cha miaka mitano umeendelea kukua hivyo ndani ya miaka 30 utabaki kuwa endelevu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Anselimu Peter amesema mfuko huo un idadi ya wanachama 24,952 na kusisitiza tathmini zinaonyesha kuwa utaendelea kuwa imara kama waajiri wataendelea kuzingatia uchangiaji wa michango ya waajiriwa wao.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini Dkt. Abdulsalaam Omar amesema sekta ya umma huchangia asilimia 0.5 kwa waajiri huku sekta binafsi ikichangia 0.6 na kwamba shughuli za sekta ziko za katika hali hatarishi ukilinganisha na umma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post