RAIS WA MALI ASHAMBULIWA KWA KISU MSIKITINI

Rais Assimi Goïta (aliyeva kanzu ya bluu) kabla ya shambulio

AFP imesambaza picha ya kanali Goita akipunga mkono baada ya tukio

***
Rais wa Mali Assimi Goïta ni 'salama' baada ya mshambuliaji aliyekuwa amejihami kwa kisu kumshambulia katika msikiti uliopo katika mji mkuu , Bamako, imesema ofisi yake.

Mwandishi wa habari wa AFP aliyekuwa katika msikiti wa Bamako-Grande Mosque ambako Kanali Goïta alikuwa amejiunga na waumini kwa ajili ya ibada ya Idd ul-Adha amesema kuwa alishambuliwa na wanaume wawili, lakini ni mmoja aliyekuwa amejihami kwa kisu.

Taarifa ya ofisi ya rais imesema kuwa mshambuliaji alikamatwa mara moja na rais aliondoshwa msikitini kwa gari mara moja hadi katika kambi za jeshi zilizopo nje ya jiji .


Waziri amelielezea shambulio hilo kama jaribio dhidi ya maisha ya rais.

Umati mkubwa ulikuwa umekusanyika katia msikiti kwa ajili ya sala, ya Idd ya kuchinja kafala.

Wengi waliisali kwenye viwanja vya msikitiImage caption: Wengi waliisali kwenye viwanja vya msikiti

Kondoo alitolewa kafara na Imam mwisho wa sala.

Shambulio linatia hofu kwa nchi inayokabiliwa na changamoto za kiusalama, ikiwa ni pamoja na uasi wa makundi ya jihad yanayofanya mashambulio ya mara kwa mara ya makundi yenye uhusiano naal-Qaeda na Islamic State

Kanali Goïta ni mtu mwenye utata – kwa kufanya mapinduzi mawili ya kijeshi chini ya mwaka mmoja .

Alijitangaza kama rais mwezi Mei baada ya kuiondoa mamlakani serikali iliyokuwa imewekwa baada ya kuongoza mapinduzi dhidi ya rais wa zamani Ibrahim Boubacar Keïta mwezi Agosti mwaka jana.

Aliahidi kuirejesha nchi katika utawala kamili wa kiraia mapema mwaka ujao.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments