MWANAFUNZI WA USC ALYANZ NASSER NA ARI YA KUBADILISHA MAZINGIRA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Tuesday, July 13, 2021

MWANAFUNZI WA USC ALYANZ NASSER NA ARI YA KUBADILISHA MAZINGIRA

Mwanafunzi wa mwaka wa pili wa chuo cha University of Southern California (USC), Alyanz Nasser alizindua maonyesho maalum tarehe 19 Juni 2021 Alliance Francaise jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.

Maonesho hayo ya yaliandaliwa na taasisi ya The Foundation for the Educational and Environment Advancement of Tanzanians (FEET). Maonyesho hayo yalileta hamasa kubwa na kudhihirisha ni kwa jinsi gani uharibifu wa mazingira ulivyo ni hatari duniani.

 Hayo yote yaliambatana na maonyesho ya picha kutoka kwa wanafunzi mbalimbali wa hapa nchini Tanzania, ikionyesha jinsi uchafu wa plastiki ulivyo kwa maisha ya kila siku ya mwanadamu pamoja na mazingira anayoishi.

Hayo yote yalifanyika kwa ufanisi mkubwa na aliyekuwa nyuma ya maonyesho haya ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa chuo cha University of Southern California (USC), Alyanz Nasser.

Alyanz Nasser amekuwa na muamko na hamasa ya kutunza mazingira tangu akiwa na umri wa miaka 15. Yeye pamoja na rafiki yake walizindua mfuko maalum ambao ni rafiki kwa mazingira unaoitwa Envirobags.

FEET ilianzisha kampeni wiki 12 zilizopita kwenye Instagram kwa lengo la kupasa sauti kwa vijana wakati huu wa mabadiliko ya tabia nchi ukiendelea. Zaidi ya shule 100 zilishiriki na wanafunzi walikuwa wakichukua picha mnato pamoja na za video kwenye maeneo ya karibu nao ambayo yanaonyesha uharibifu wa mazingira.

 Nia ya kampeni hii ilikuwa ni kutoa hamasa na kuonyesha ni kwa jinsi ngani binadamu wanaharifu mazingira na jinsi wanafunzi wanaweza kushiriki kubadilisha hali hiyo.

FEET pia itapanda miti 20,000 aina ya Jacaranda hapa Tanzania. Juhudi hizi zitasaidia jamii ya Tanzania kwa kusaidia kuongeza hali nzuri ya mazingira, upungufu wa chakula pamoja na kuongeza kipato. Njaa, ukataji holela wa miti, upungufu wa chakula, ushindani wa mali asili, njaa na uhamiaji halole na haramu zimechangia sana uharibifu wa mazingira. Miti ni mali asili ambayo itatatua changamoto zote hizo.

FEET pia ina mpango wa kupanda asilia ambayo usaidia kuimarisha ardhi na kuifanya iwe na faida Zaidi na imara na hivyo kuongeza bioanuwai, wakati mbinu salama za kilimo zikihimiza kilimo endelevu pamoja na utafutaji wa maisha.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Liberata Mulamula, Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Ummy Mwalimu, Balozi wa Ufaransa hapa nchini Frederic Clavier, Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Raisi Dkt Andrew Komba pamoja na mabalozi watatu wa mazingira walikuwepo.

Waziri Liberata Mulamula alisema, ‘Utunzaji wa mazingira, uwe mdogo au mkubwa ukindwa kwa pamoja utasaidia kubadilisha maisha ya binadamu wanaotengemea mazingira. Nakushukuru kwa vile unavyofanya na vile imesaidia nchi kwenye kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Umechangua njia sahihi. Nawapongeza FEET pamoja na washirika wake.’

Waziri Ummy Mwalimu alisema, ‘Tunayo taarifa kwamba FEET itapanda miti 20,000, tutafanya kazi pamoja nanyi kama serikali za mtaa kuhakikisha kuwa lengo lenu linafanikiwa’.

Balozi Frederic Clavier pia alitoa pongezi kwa FEET, ‘Sisi kwa pamoja tunatakiwa kufanya kazi kulinda mazingira yetu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, ukataji ovyo wa miti pamoja na uchafuzi wa mazingira’.

Mkurugenzi wa Mazingira Dkt Andrew Komba alisema kuwa anatambua juhudi za kila mtu za kulinda mazingira pamoja na kupambana na uchafuzi wa mazingira.
Honorable Minister Liberata Mulamula delivering a speech at FEET's Ecosystem Restoration Campaign Launch.
Alyanz Nasser - FEET founder delivering a speech at the Ecosystem Restoration Campaign
From Left to Right:His Excellency Frederic Clavier, Honorable Minister Ummy Mwalimu, Alyanz Nasser - FEET Founder, Mariam Ditopile Environment Ambassador, at the FEET event.
Alyanz explaining the purpose of the exhibition to the VIP guests.
Alyanz with his tutor Moses in the Exhibition Hall
School Students who were the winners of FEET's ecosystem restoration campaign

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages